Jeshi
la Polisi Zanzibar linamshikilia Askari mmoja wa Chuo cha Mafunzo aliyesimamia
kunyolewa ndevu kwa viongozi wa jumuiya na taasisi zakiislam Zanzibar ambao
wako rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa bila ya kesi yao kutolewa hukumu.
Askari
huyo amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa shilingi 1,635,000 alizoziiba kutoka
katika duka moja lililopo katika eneo la Makadara mjini Zanzibar.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Mkadam Khamis Mkadam, amemtaja
Askari huyo kuwa ni Sajin Meja (S/Sgt) Hassan Iddi
Hassan (45), wa Chuo cha Mafunzo Makao Makuu.
Kamanda
Mkadam amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.00 jioni ambapo
Askari huyo akiwa amevaa kiraia, alifika dukani hapo kama mteja wa kawaida na
wakati muuzaji wa duka hilo akimhudumia mteja mwingine upande wa pili, aliingia
ndani na kukimbilia kwenye droo ya pesa na
kuzichukua fedha hizo na kuondoka.
Amesema kuwa wakati akichukua fedha hizo, Askari huyo alionekana
na baadhi ya wateja na hivyo kumshitua muuzaji huyo na kuanza kupiga kelele za
mwizi na ndipo alipofukuzwa na wananchi ambapo eneo hilo lilikuwa karibu na Kituo
cha Polisi na askari waliwahi haraka na kumkamatwa kabla ya kupata kipigo
kikali kutoka kwa wananchi.
Kamanda
Mkadam, amesema fedha zote alizokua ameziiba mtuhumiwa huyo zimeokolewa na
Polisi na zimehifadhiwa kama kielelezo mahakamani.
Hilo
ni tukio la tatu kutokea
mjini Zanzibar katika kipindi cha mwaka huu ambapo tukio la kwanza ni lile la
jaribio la wizi katika maghala ya Bakheresa eneo la Fuoni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa wakiwa na silaha aina ya gobore
linalotumia risasi za short gun.
Na
tukio lingine ni la kukamtwa kwa majambazi wane akiwemo Afisa wa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa nchini wakiwa na silaha tatu zikiwemo bastola mbili na
SMG moja baada ya kumvamia mfanyabiashara mmoja na kumpora milioni 11.5 eneo
la Rahaleo mjini Zanzibar.
Matukio
hayo yote yakiwa na jumla ya watuhumiwa wanane na silaha nne yaliweza
kukabiliwa kwa haraka na Polisi kufuatia msaada wa wananchi wa kutoa taarifa za
haraka polisi na wenyewe kujitolea kusaidiana na Polisi kuwakabili watuhumiwa
na kufanikisha ukamataji salama.
Wakizungumza
na mizani baadhi ya waislam wamesema kuwa dua zao walizokuwa wakisoma
kumshtakia mwenyezi Mungu kutokana na vitendo vya dhulma wanavyofanyiwa zinaendelea
kukubaliwa.
No comments:
Post a Comment