CAIRO
SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA BINAADAMU
LA AMNESTY INTERNATIONAL LIMEKOSOA VIKALI UKATILI WA VIKOSI VYA USALAMA VYA
MISRI DHIDI YA WAANDAMANAJI WANAOMUUNGA MKONO RAIS ALIYEONDOLEWA MADARAKANI
MUHAMMAD MORSI.
KATIKA RIPOTI ILIYOTOLEWA JANA
JUMATANO KABLA YA MAADHIMISHO YA MWAKA WA TATU WA MAPINDUZI YA WANANCHI MWAKA
2011 YALIYOMUONDOA MADARAKANI DIKTETA HOSNI MUBARAK, AMNESTY IMESEMA WATAWALA
WA MISRI WANATUMIA KILA NJIA INAYOWEZEKANA KUWAKANDAMIZA WAPINZANI NA KUKIUKA
HAKI ZA BINAADAMU.
MKUU WA AMNESTY INTERNATIONAL
MASHARIKI YA KATI NA AFRIKA KASKAZINI HASSIBA HADJ SAHRAOU AMESEMA 'BAADA YA
KUPITA MIAKA MITATU, MATAKWA YA 'MAPINDUZI YA JANUARI 25' YA KUTAKA KUHESHIMIWA
HAKI ZA BINAADAMU HAYAJAFIKIWA.
WATU KADHAA WALIOONGOZA MAPINDUZI
HAYO WAKO KOROKORONI HUKU UKANDAMIZAJI NA UKIUKAJI SHERIA UKIWA JAMBO LA
KAWAIDA.' SHIRIKA HILO LA KUTETEA HAKI ZA BINAADAMU LIMEONGEZA KUWA WATU 1,400
WAMEUAWA NA VIKOSI VYA USALAMA KATIKA MACHAFUKO YA KISIASA YALIYOANZA JULAI 3
MWAKA JANA BAADA YA JESHI KUMUONDOA MADARAKANI MORSI.
WAFUASI WA MORSI WAMEKUWA
WAKIANDAMANA MARA KWA MARA WAKITAKA AREJESHWE MADARAKANI.
No comments:
Post a Comment