RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS WA INDIA MHESHIMIWA SHRI
PRANAB MUKHERJEE KWA KUADHIMISHA MIAKA 65 YA UHURU WA NCHI HIYO.
KATIKA SALAMU ZAKE HIZO, DK. SHEIN AMESEMA WANANCHI WA
ZANZIBAR WANAUNGANA NA NDUGU ZAO WA INDIA KUSHEREHEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
WALIYOYAPATA KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIAKA 65 YA UHURU.
“TUNAUPONGEZA NA KUTHAMINI UHUSIANO ULIOPO KATI YA
NCHI ZETU AMBAO UNAZIDI KUIMARIKA SIKU HADI SIKU NA TUNAELEZA DHAMIRA YETU YA
DHATI YA KUPANUA USHIRIKIANO HUO KATIKA MAENEO YA UCHUMI, BIASHARA, UTAMADUNI
NA MASUALA YA UFUNDI NA UHUSIANO WA KIMAITAIFA” DK. SHEIN AMEELEZA KATIKA
SALAMU HIZO.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
AMEITUMIA FURSA HIYO KUMTAKIA RAIS MUKHERJEE AFYA NJEMA NA MAISHA YENYE FURAHA.
No comments:
Post a Comment