WILAYA YA KUSINI UNGUJA
WAKULIMA WA MWANI WAMEYAOMBA MAKAMPUNI YA
KUNUNUA MWANI KUANDAA UTARATIBU MAALUM WA KUWAONGEZEA BEI YA BIDHAA HIYO ILI WAWEZA
KUENDELEZA NA KUBORESHA ZAO HILO NCHINI.
WAKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO MMOJA YA
WAKULIMA HAO BI MTUMWA SULEIMANI KHAMIS HUKO MAKUNDUCHI WILAYA YA
KUSINI,AMESEMA WAKULIMA WA MWANI WANAKATA TAMAA YA KUENDELEZA KILIMO HICHO
KUTOKANA NA BEI YA MWANI KUWA NDOGO.
WAMESEMA LICHA YA KUONGEZEKA JITIHADA ZA
KUENDELEA KULIMA ZAO HILO LAKINI KUTOKANA NA BEI NDOGO YA ZAO HILO
LIMEWASABABISHIA KUACHA KULIMA ZAO HILO.
KWA UPANDE WAKE MNUNUZI WA MWANI KITUO CHA
MAKUNDUCHI NDUGU KHATIBU ABDAALLAH OMARI AMESEMA MWANI NI BIASHARA AMBAYO
HUUZWA NJE YA NCHI NA INATUMIA GHARAMA KUBWA HADI KUFIKA KATIKA SOKO JAMBO
AMBALO LINAWAPELEKEA KUTOKUZIDISHA BEI YA ZAO HILO.
HATA HIVYO AMEIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA USHURU KWA MAKAMPUNI YANAYOSAFIRISHA MWANI
MWANI ILI WAWEZE KUONGEZA BEI KWA WAKULIMA WA ZAO HILO.
No comments:
Post a Comment