ZANZIBAR
RAIS WA ZANZIBAR AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA
BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN JANA AMEKUTANA NA WAZIRI MKUU WA
FINLAND BWANA JYRKI KATAINEN NA KUFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU UHUSIANO NA
USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA FINLAND.
KATIKA MAZUNGUMZO
HAYO YALIYOFANYIKA IKULU ZANZIBAR DK. SHEIN AMEISHUKURU SERIKALI YA FINLAND KWA
MISAADA YAKE MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA IKIITOA KWA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA
JUMLA.
ALIBAINISHA
KUWA UHUSIANO MZURI KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA FINLAND
IMEIWEZESHA ZANZIBAR KUPOKEA MISAADA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO,
HUDUMA ZA JAMII NA HIFADHI YA MAZINGIRA.
DK. SHEIN
ALIELEZA KUFURAHISHWA KWAKE NA UAMUZI WA SERIKALI YA FINLAND KUENDELEZA
USHIRIKIANO WAKE NA ZANZIBAR KWA KUENDELEZA MRADI WA UHIFADHI WA ARDHI NA
MAZINGIRA KWA AWAMU YA PILI (SMOLE II) BAADA YA KUMALIZIKA KWA AWAMU YA KWANZA.
HATA HIVYO
RAISI WA ZANZIBAR AMEKARIBISHA WAZO LA KUSHIRIKIANA NA FINLAND KATIKA
KUTEKELEZA AZMA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUTAFUTA NJIA MBADALA ZA
KUPATA NISHATI YA UMEME.
ALIELEZA
KUWA NI KWELI HIVI SASA ZANZIBAR INAPATA UMEME WA KUTOSHA KUPITIA MKONGA WA
UMEME TOKA TANZANIA BARA LAKINI HAITAKUWA AJABU BAADA YA MIAKA MICHACHE IJAYO
KUTOKANA NA KASI YA ONGEZEKO LA MATUMIZI YA UMEME YANAYOTAKANA NA KASI YA
UKUAJI WA UCHUMI KIASI KILICHOPO SASA KIKAWA HAKITOSHI HIVYO NI JAMBO LA BUSARA
KUWA NA MPANGO MBADALA WA KUPATA NISHATI HIYO.
WAKATI
HUO HUO
WAZIRI MKUU WA FINLAND BWANA JYRKI KATAINEN AMEMPONGEZA RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWA MAFANIKIO ALIYOYAPATA KATIKA KUIONGOZA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ILIYO CHINI YA MFUMO UMOJA WA KITAIFA.
AMESEMA
MFUMO HUO UNASAIDIA KULETA MAELEWANO BAINA YA VYAMA NA UZOEFU UNAONYESHA KUWA
UTAMADUNI WA UENDESHAJI WA SERIKALI KWA MFUMO KAMA HUO NA MINGINE INAYOFANANA
NA HUO UNATUMIKA SANA HIVI SASA.
No comments:
Post a Comment