MKOA WA KASKAZINI UNGUJA
JUMALA YA MATUKIO SABINI NA MOJA YA AJALI ZA
BARABARANI YAMERIPOTIWA KUTOKEA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KATIKA KIPINDI CHA
MWAKA 2013.
AKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA HASSAN MSANGI AMESEMA KUTOKANA NA KUWEPO KWA
HALI YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA BARABARANI KWA BAADHI YA MADEREVA KUMEPELEKEA ZAIDI YA WATU ISHIRINI KUPOTEZA
MAISHA NA WENGINE KUPATA ULEMAVU WA VIUNGO.
AKIYATAJA MAENEO YALIYOONGOZA KWA MATUKIO YA
AJALI ZA BARABARANI NI PAMOJA NA KAZOLE,MGAMBO,MKWAJUNI NA NUNGWI.
AMEFAHAMISHA KUWA KWA SASA JESHI LA POLISI LIMEIMARISHA
ULINZI ZAIDI KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MKOA HUO KWA LENGO LA KUEPUSHA AJALI
ZA BARABARANI.
SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA MADEREVA WAWE
WAANGALIFU NA KUFUATA SHERIA BILA YA KUSHURUTISHWA SAMBAMBA NA KUZINGATIA ALAMA
ZA BARABARANI ILI KUWAEPUSHIA USUMBUFU WATEMBEA KWA MIGUU.
No comments:
Post a Comment