tangazo

tangazo

Thursday, January 30, 2014


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR NA INDIA UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU AMBAPO WAKATI WOTE PANDE MBILI HIZO ZIMEKUWA ZIKIFANYA JITIHADA ZA KUONA USHIRIKIANO HUO UNALETA TIJA ZAIDI KWA KILA UPANDE.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA BALOZI MDOGO WA INDIA BWANA PAWAN KUMAR AMBAYE ALIFIKIA IKULU KUMUAGA RAIS BAADA YA KUMALIZA KIPINDI CHAKE CHA KUITUMIKIA NCHI YAKE HUMU NCHINI.

AMEBAINISHA KUWA TANGU UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA ULIPOANZISHWA MIAKA YA SITINI NCHI HIZO ZIMESHUHUDIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UHUSIANO HUO HUKU PANDE HIZO ZIKISHIRIKIANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO ELIMU.

ALIONGEZA KUWA AMEFARAJIKA KUONA KUWA KATIKA KIPINDI HICHO HASUSAN KATIKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI WATUMISHI WENGI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAMEPATA FURSA ZA MASOMO KWA MSAADA WA NCHI HIYO KWA MAFUNZO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU.

DK. SHEIN ALISISITIZA KUWA HISTORIA YA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA INDIA UMEDUMU KWA KARNE NYINGI HIVYO KUNA KILA SABABU KUONA KUWA HISTORIA HIYO INAENDELEZWA KWA KUZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MENGI ZAIDI.

ALIMSHUKURU BALOZI KUMAR KWA KUTEKELEZA VYEMA MAJUKUMU YAKE AKIITUMIKIA NCHI YAKE ZANZIBAR NA AMEKIRI KUWA KATIKA KIPINDI CHAKE AMESHUHUDIA UHUSIANO KATI YA NCHI MBILI HIZO UKISHIKA KASI KWA PANDE HIZO KUONYESHA ARI YA KUUENDELEZA NA KUUIMARISHA.

KWA UPANDE WAKE BALOZI KUMAR ALIELEZA KUWA AMEFURAHI KUPATA FURSA YA KUITUMIKIA NCHI YAKE HAPA ZANZIBAR NA KUONGEZA KUWA ANAAMINI AMETEKELEZA VYEMA JUKUMU LAKE LA KUIMARISHA UHUSIANO KATI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR LAKINI ALIKIRI KUWA NCHI MBILI HIZO ZINA FURSA ZAIDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO HUO.

WAKATI HUO HUO RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAKARIBISHA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KATIKA SEKTA YA ELIMU KWA KUTAMBUA KUWA LENGO NI KUTOA FURSA ZAIDI KWA WATOTO NA KUIMARISHA HUDUMA YA ELIMU NCHINI.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI KUTOKA NCHINI MAREKANI- OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ULIOONGOZWA NA MWANZILISHI WA TAASISI HIYO BWANA JOE RICKETTS.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMUELEZA BWANA RICKETTS KUWA AMEFURAHI KUONA KUWA TAASISI HIYO IMEAMUA KUTOA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA MUHIMU YA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO IMEELEKEZA NGUVU ZAKE KATIKA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KITOLEWACHO MASKULINI.

AMEBAINISHA KUWA NI JAMBO ZURI KUWA TAASISI HIYO IMEELEKEZA MISAADA YAKE KATIKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA KUSISITIZA KUWA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA HIZO NI JAMBO LINALOTILIWA MKAZO NA SERIKALI ANAYOINGOZA.

DK. SHEIN AMEELEZA KUWA LENGO LA TAASISI HIYO KUSAIDIA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA SKULI ZA MSINGI NA SEKONDARI NI MUHIMU KWA KUWA LINAWEKA MSINGI MZURI KWA AJILI YA ELIMU VYUO NA VYUO VIKUU.

KWA HIVYO ALIELEZA MATUMAINI YAKE KUWA USHIRIKIANO HUO UTAENDELEZWA NA AMEIHAKIKISHIA TAASISI HIYO KUWA SERIKALI ITAIPA KILA USHIRIKIANO UTAKAOUHITAJI ILI KUFANIKISHA MALENGO YA TAASISI NA TAIFA KWA JUMLA.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO AMBAYO YALIHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ALI JUMA SHAMUHUNA NA KATIBU MKUU WAKE BIBI MWANAIDI SALEH ABDALLA, DK. SHEIN ALITUMIA FURSA HIYO KUMUELEZA BWANA RICKETTS HATUA MBALIMBALI ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA KUIMARISHA ELIMU IKIWEMO UJENZI WA SKULI BORA ZA KISASA ILI KUIMARISHA UTOAJI WA ELIMU NCHINI.

KWA UPANDE WAKE BWANA JOE RICKETTS ALISEMA KUWA AMEFURAHI TAASISI YAKE KUPATA FURSA YA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZANZIBAR NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUIUNGA MKONO TAASISI HIYO NA SHUGHULI INAZOZIFANYA.

TAASISI YA OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ILIANZISHWA MWAKA 2005 LENGO LAKE LIKIWA NI KUHAKIKISHA WATOTO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA WANAPATA KIWANGO BORA CHA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO HUTOA MISAADA KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA KATIKA MASKULI.

KWA KUFANYA HIVYO TAASISI HIYO INAAMINI KUWA ITAWEZA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WATOTO WA NCHI HIZO NA KUWAJENGEA MUSTAKABLI BORA WA MAISHA YAO.

HIVI SASA KWA UPANDE WA ZANZIBAR TAASISI HIYO INATARAJIA KUGAWA VIFAA VYA TEKINOHAMA KAMA VILE TABULETI KWA WALIMU NA WANAFUNZI KATIKA BAADHI YA SKULI IKIWEMO SKULI ZA SEKONDARI ZA LAURET ILIYOPO UNGUJA NA FIDEL CASTRO HUKO PEMBA.

No comments:

Post a Comment