Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefungua kampeni
za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo, na
kuwanasihi wakaazi hao kutochagua viongozi wanaojihusisha na vitendo vya
rushwa.
Amesema
kiongozi atakayechaguliwa kwa kutoa rushwa, kamwe hatoweza kukemea vitendo
hivyo na badala yake ataviendeleza na kuwaacha wananchi wakibakia katika hali
ya umaskini na matatizo mengi katika maeneo yao.
Maalim
Seif amewashauri wakaazi hao kusikiliza sera za wagombea wote, ili waweze
kuzipima na kuzichambua na hatimaye kuchagua kiongozi atakayewajali na kusaidia
kuwatatulia kero zinazowakabili.
Amesema
mgombea wa CUF katika kata hiyo nd. Njema Seif Mohd, ameonesha dalili njema kwa
kuwa mwaminifu na mtu anayewajali wenzake, na kuwataka wakaazi hao kutofanya
makosa katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 mwezi ujao.
Kwa
upande wake, mgombea wa udiwani CUF katika kata hiyo ya Magomeni Wilayani
Bagamoyo nd. Njema Seif Mohd ameahidi kusimamia matatizo yanayowakabili wakaazi
hao kwa lengo ya kuyatafutia ufumbuzi.
Akitaja
vipaumbele vyake amesema atasimamia suala la elimu ili kuhakikisha kuwa watoto
wote wanakwenda skuli bila ya vikwazo vyovyote, pamoja na kusimamia upatikanaji
wa vifaa vya hospitali ikiwa ni pamoja na madawa.
Aidha
amesema atasimamia mapato ya halmashauri hiyo ili kuona kuwa yanatumika kama
yalivyokusudiwa.
“Nichagueni
tutetee Magomeni yetu”, alijinadi Njema.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Julius
Mtatiro, alishutumua utendaji wa halmashauri hiyo na kudai kuwepo kwa matumizi
mabaya ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment