ZANZIBAR.
JUMLA YA
WAISLAM 300 WAKIKE NA KIUME
KUTOKA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAMEWATEMBELEA WAKE WA VIONGOZI
WAHARAKATI YA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM
ZANZIBAR KATIKA MSIKITI WA MBUYUNI MJINI ZANZIBAR.
WAISLAM HAO WAMEPOKEWA NA MLEZI WA JUMUIYA
YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AMIRI HAJJI KHAMIS HAJJI AMBAYE ALIKUWA PAMOJA NA WAKE WA
VIONGOZI HAO MSIKITINI HAPO.
WAISLAM HAO WAMEKABIDHI VYAKULA MBALI MBALI KWA WAKE WA VIONGOZI HAO
ZIKIWEMO FEDHA TASLIM SHILINGI LAKI
NANE.
NAYE AMIRA WA WAKE WA VIONGOZI HAO
UKHTI SADA AMESEMA KUWA WAMEFARIJIKA
NA SUALA LAKUWATEMBELEWA NA UJUMBE HUO
KUTOKA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA .
No comments:
Post a Comment