WILAYA YA MAGHARIBI.
Wapigakura Wa Jimbo La Kiembesamaki Wametakiwa Kumchagua Mgombea Wa Chama Cha
Tadea Ili Kuondoa Tatizo La Unyanyasaji Wakijinsia Kwa Akinamama Na Watoto.
Akifungua Kampeni Za Uchaguzi Mdogo Wa Jimbo
La Kiembesamaki Katibu Mkuu Wa Tadea Juma Ali Khatibuwakati Akizungumza Katika
Viwanja Vya Kisima Mbaazi.
Amesema Kuwa Jimbo La Kiembesamaki Lina
Rasilimali Za Ajira Ambazo Hadi Sasa Hazijafanyiwakazi Hivyo Iwapo Atachaguliwa
Mgombea Wa Chama Hicho Ndugu Ali Mohd Mbongo Ataleta Maendeleo Hayo.
Aidha Ndugu Juma Amebainisha Kuwa Chama Chake
Kitaangalia Wananchi Wote Wa Hali Za Chini Ili Kuhakikisha Kuwa Wanapata Huduma
Zote Muhimu Ndani Ya Kipindi Cha Miezi Mitatu Iwapo Tadea Itapewa Ridhaa.
Amewataka Wakaazi Wa Kiembesamaki Kukichagua
Chama Chake Ili Kuhakikisha Kinawaunganisha Wajasiriamali Nakuwapatia Maji
Safi Na Salama Katika Jimbo Hilo.
Nae Mgombea Uwakilishi Wan Jimbo La Kiembe
Samaki Kupitia Chama Cha Tadea Ali Mohd Mbongo Amewataka Wananchi Hao Kumpa
Kura Za Ndio Ili Aweze Kuimarisha Dhana Ya Polisi Jamii Ndani Ya Jimbo La
Kiembe Samaki Na Kuwalipa Mishahara Sambamba Na Kushughulikia Vituo Vya Afya
Kila Shehia Ndani Ya Jimbo Hilo.
No comments:
Post a Comment