tangazo

tangazo

Monday, January 20, 2014

KUSINI UNGUJA

MKOA  WA  KUSINI.
                KATIKA KUDHIBITI WIMBI LA  KUWEPO KWA VIKUNDI VIOVU KATIKA MKOA WA KUSINI UONGOZI WA MKOA  HUO UMEANZISHA DARASA MAALUMU LA VIJANA ILI KUWEZA KUJIPATIA ELIMU AMBAYO ITAWEZA KUWAEPUSHA KUJIINGIZA KATIKA  VIKUNDI HIVYO.
                AKIZUNGUMZA NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR AFISA  TAWALA WA  MKOA WA WAKUSINI ABDALLA ALI KOMBO AMESEMA KUWA ELIMU HIYO ITAWASAIDIA ZAIDI VIJANA KATIKA KUELIMIKA JUU YA KUONDOKANA NA VITENDO VIOVU AMBAVYO VINAWEZA KUSABABISHA KUPOTEA KWA AMANI YA NCHI.
                AMESEMA KUWA KATIKA KULIANDAA DARASA HILO WAMEPOKEA WALIMU I5 KUTOKA SWIDEN NDANI YA MANISPAA YA KIRUNA AMBAO WATAWEZA KUSOMESHA MASOMO YA SAYANSI ,COMPYUTA, ENGLISH AMBAYO YATAWEZA KUWAJENGEA UWEZO WA KUJIAJIRI WENYEWE ILI KUONDOKANA NA WIMBI LA VIJANA WASIO NA AJIRA KATIKA MKOA HUO.
                AMEFAHAMISHA KUWA MASOMO HAYO AMBAYO YANATARAJIWA KUANZA HIVI KARIBUNI YA YATAWEZA KUWASHIRIKISHA VIJANA  12  AMBAO WATASOMA MASOMO YASAYANSI NA KWA MASOMO MENGINE WATAWASHIRIKISHA VIJANA  WOTE WA MKOA  HUO ILI KUWEZA KUFAIDIKA NA MASOMO HAYO.

                HIVYO AMEWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA MADARASA HAYO ILI KUWEZA KUJIPATIA ELIMU AMBAYO ITAWEZA KUTOLEWA BILA YA MALIPO NA KUWEZA KUWAPA MASHIRIKIANO WALIMU KUTOKA SWIDEN  WALIOKUJA KUJITOLEA KATIKA KUWAPA ELIMU VIJANA WOTE  WA  MKOA WA  KUSINI.

No comments:

Post a Comment