ZANZIBAR.
SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR (ZECO) LIMESEMA KUWA
LINAKUSUDIA KUPANDISHA TENA BEI YA UMEME BAADA YA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA
ZA NISHATI NA MAJI (EWURA) KULIRUHUSU SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
KUONGEZA BEI YA UMEME.
AKIZUNGUMZIA SUALA HILO MENEJA WA SHIRIKA LA
UMEME ZANZIBAR, NDUGU HASSAN ALI MBAROUK, AMESEMA KUWA TARATIBU ZA KUONGEZA BEI
YA UMEME ZINAFANYWA, AMBAPO HADI SASA MALIPO HAYO MAPYA HAIJAFAHAMIKA YATAANZA
LINI.
AMESEMA KUWA KWA SASA WATEJA WA SHIRIKA HILO
WATAENDELEA KULIPA BEI YA SASA WAKATI SHIRIKA LIKIENDELEA NA UTARATIBU WA
KUWEKA BEI MPYA.
BEI HIYO MPYA INAKUJA WAKATI HIVI KARIBUNI
SHIRIKA HILO LILIPANDISHA GHARAMA ZA HUDUMA ZA UMEME, AMBAZO ZINALALAMIKIWA NA
WATEJA.
AMESEMA KUWA BEI HIYO MPYA, INAWEZA KUWASHTUA
WATEJA, NA NDIO HALI YA BIASHARA NA KWAMBA ZECO HAINA BUDI KURIDHIA MABADILIKO
HAYO.
AMEWATAKA WATEJA KUTUMIA UMEME KWA UANGALIFU
ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA.
HIVI KARIBUNI, MKURUGENZI MDHIBITI UCHUMI WA
EWURA, ND. FELIX NGAMLAGOSI,ALITANGAZA RASMI ONGEZEKO LA GHARAMA ZA UMEME KWA
ASILIMIA 50 GHARAMA AMBAZO ZILIANZA KUTUMIKA RASMI JANUARI MOSI 2014.
No comments:
Post a Comment