Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim
Seif Sharif Hamad, amefika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwajuilia
hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali
Suleiman, pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya waliolazwa
katika hospitali hiyo.
viongozi hao wamelazwa katika hospitali hiyo
wakisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Wakizungumza na Makamo wa Kwanza wa Rais,
wamesema wanaendelea vizuri na kwamba afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi
siku, tofauti na walipofikishwa hospitalini hapo.
Waziri Haroun anatarajiwa kupelekwa nchi Afrika
ya Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewaombea viongozi hao wapone haraka ili
waendelee na majukumu ya kulitumikia taifa.
MNAENDELEA KUSKILIZA TAARIFA HII YA KHABARI KUTOKA RADIO
ADHANA FM MASJID JUMUIYA RAHALEO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment