PEMBA.
WATU nane wakiwemo mabaharia wanne, wamenusurika kifo baada ya
jahazi walilokuwa wakisafiria kutoka Tanga kwenda Wete Pemba, kukumbwa na upepo
mkali na kulazimika kumwaga mzigo waliokua wamepakia.
Kadhia hiyo iliwakumba tarehe 16 mwezi majira ya saa 8:50 mchana,
wakati jahazi hiyo ikiwa imebeba bidhaa za aina mbali mbali za wafanyabiashara
wa miji ya Pemba.
Baadhi ya mabaharia waliokuwemo kwenye chombo hicho, walisema
waliondoka bandari ya Tanga wakiwa salama na kwamba mzigo waliobeba ulikuwa wa
kawaida, lakini hali ilibadilika kadiri safari ilivyoendelea.
Walisema walibeba matenga ya tungule 300, viazi mbatata gunia 30,
vituguu maji gunia 40, magodoro 30 pamoja na vitu vyengine vidogo vidogo kama
mafuta ya kupikia, madumu, misumari na mapipa matupu.
Mmoja kati ya mabaharia hao aliejitambulisha kwa jina moja la
Mohamed (Mudi) alisema, wakati wako nusu ya safari yao, ulitokezea upepo usio
wa kawaida na kuliyumbisha jahazi lao.
No comments:
Post a Comment