RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA
UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR NA INDIA
UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU AMBAPO WAKATI WOTE PANDE MBILI HIZO ZIMEKUWA
ZIKIFANYA JITIHADA ZA KUONA USHIRIKIANO HUO UNALETA TIJA ZAIDI KWA KILA UPANDE.
DK. SHEIN
AMESEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA BALOZI MDOGO WA INDIA BWANA PAWAN
KUMAR AMBAYE ALIFIKIA IKULU KUMUAGA RAIS BAADA YA KUMALIZA KIPINDI CHAKE CHA
KUITUMIKIA NCHI YAKE HUMU NCHINI.
AMEBAINISHA
KUWA TANGU UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA ULIPOANZISHWA MIAKA YA SITINI NCHI HIZO
ZIMESHUHUDIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UHUSIANO HUO HUKU PANDE HIZO
ZIKISHIRIKIANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO ELIMU.
ALIONGEZA
KUWA AMEFARAJIKA KUONA KUWA KATIKA KIPINDI HICHO HASUSAN KATIKA MIAKA YA HIVI
KARIBUNI WATUMISHI WENGI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAMEPATA FURSA ZA
MASOMO KWA MSAADA WA NCHI HIYO KWA MAFUNZO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU.
DK. SHEIN
ALISISITIZA KUWA HISTORIA YA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA
INDIA UMEDUMU KWA KARNE NYINGI HIVYO KUNA KILA SABABU KUONA KUWA HISTORIA HIYO
INAENDELEZWA KWA KUZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MENGI ZAIDI.
ALIMSHUKURU
BALOZI KUMAR KWA KUTEKELEZA VYEMA MAJUKUMU YAKE AKIITUMIKIA NCHI YAKE ZANZIBAR
NA AMEKIRI KUWA KATIKA KIPINDI CHAKE AMESHUHUDIA UHUSIANO KATI YA NCHI MBILI
HIZO UKISHIKA KASI KWA PANDE HIZO KUONYESHA ARI YA KUUENDELEZA NA KUUIMARISHA.
KWA UPANDE
WAKE BALOZI KUMAR ALIELEZA KUWA AMEFURAHI KUPATA FURSA YA KUITUMIKIA NCHI YAKE
HAPA ZANZIBAR NA KUONGEZA KUWA ANAAMINI AMETEKELEZA VYEMA JUKUMU LAKE LA
KUIMARISHA UHUSIANO KATI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR LAKINI ALIKIRI KUWA NCHI
MBILI HIZO ZINA FURSA ZAIDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO HUO.
WAKATI
HUO HUO
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN
AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAKARIBISHA USHIRIKIANO KATI YA
SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KATIKA SEKTA YA ELIMU KWA KUTAMBUA KUWA LENGO NI KUTOA
FURSA ZAIDI KWA WATOTO NA KUIMARISHA HUDUMA YA ELIMU NCHINI.
DK. SHEIN
AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI ISIYO YA
KISERIKALI KUTOKA NCHINI MAREKANI- OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION
ULIOONGOZWA NA MWANZILISHI WA TAASISI HIYO BWANA JOE RICKETTS.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMUELEZA BWANA RICKETTS KUWA AMEFURAHI KUONA KUWA
TAASISI HIYO IMEAMUA KUTOA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA MUHIMU YA ELIMU AMBAPO
TAASISI HIYO IMEELEKEZA NGUVU ZAKE KATIKA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU
KITOLEWACHO MASKULINI.
AMEBAINISHA
KUWA NI JAMBO ZURI KUWA TAASISI HIYO IMEELEKEZA MISAADA YAKE KATIKA SEKTA YA
UMMA NA BINAFSI NA KUSISITIZA KUWA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA HIZO NI JAMBO
LINALOTILIWA MKAZO NA SERIKALI ANAYOINGOZA.
DK. SHEIN
AMEELEZA KUWA LENGO LA TAASISI HIYO KUSAIDIA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU
KATIKA SKULI ZA MSINGI NA SEKONDARI NI MUHIMU KWA KUWA LINAWEKA MSINGI MZURI
KWA AJILI YA ELIMU VYUO NA VYUO VIKUU.
KWA HIVYO
ALIELEZA MATUMAINI YAKE KUWA USHIRIKIANO HUO UTAENDELEZWA NA AMEIHAKIKISHIA
TAASISI HIYO KUWA SERIKALI ITAIPA KILA USHIRIKIANO UTAKAOUHITAJI ILI
KUFANIKISHA MALENGO YA TAASISI NA TAIFA KWA JUMLA.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO AMBAYO YALIHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
ALI JUMA SHAMUHUNA NA KATIBU MKUU WAKE BIBI MWANAIDI SALEH ABDALLA, DK. SHEIN
ALITUMIA FURSA HIYO KUMUELEZA BWANA RICKETTS HATUA MBALIMBALI ZINAZOCHUKULIWA
NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA KUIMARISHA ELIMU IKIWEMO UJENZI WA
SKULI BORA ZA KISASA ILI KUIMARISHA UTOAJI WA ELIMU NCHINI.
KWA UPANDE
WAKE BWANA JOE RICKETTS ALISEMA KUWA AMEFURAHI TAASISI YAKE KUPATA FURSA YA
KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZANZIBAR NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUIUNGA MKONO
TAASISI HIYO NA SHUGHULI INAZOZIFANYA.
TAASISI YA OPPORTUNITY
EDUCATION FOUNDATION ILIANZISHWA MWAKA 2005 LENGO LAKE LIKIWA NI
KUHAKIKISHA WATOTO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA WANAPATA KIWANGO BORA CHA ELIMU
AMBAPO TAASISI HIYO HUTOA MISAADA KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHA NA
KUJIFUNZA KATIKA MASKULI.
KWA KUFANYA
HIVYO TAASISI HIYO INAAMINI KUWA ITAWEZA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WATOTO
WA NCHI HIZO NA KUWAJENGEA MUSTAKABLI BORA WA MAISHA YAO.
HIVI SASA
KWA UPANDE WA ZANZIBAR TAASISI HIYO INATARAJIA KUGAWA VIFAA VYA TEKINOHAMA KAMA
VILE TABULETI KWA WALIMU NA WANAFUNZI KATIKA BAADHI YA SKULI
IKIWEMO SKULI ZA SEKONDARI ZA LAURET ILIYOPO UNGUJA NA FIDEL CASTRO HUKO PEMBA.
No comments:
Post a Comment