RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEKUTANA
NA WAZIRI WA FEDHA WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA
SAADA MKUYA SALUM.
WAZIRI SAADA
ALIFIKA IKULU KUJITAMBULISHA RASMI YEYE NA MANAIBU WAKE ADAM KIGOMA ALI MALIMA
NA MWIGULU LAMECK NCHEMBA KUFUATIA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI
YALIYOFANYWA HIVI KARIBUNI NA RAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA
MRISHO KIKWETE AMBAPO MABADILIKO HAYO YALIIGUSA WIZARA HIYO.
KATIKA
MAZUNGUMZO YAKE NA WAZIRI HUYO NA UJUMBE WAKE DK. SHEIN ALISISITIZA UMUHIMU WA
USHIRIKIANO NA UTENDAJI KAZI WA PAMOJA ILI KUKIDHI MATARAJIO YA SERIKALI PAMOJA
NA MATUMAINI MAKUBWA WALIYONAYO WATANZANIA KWAO.
ALIELEZA
KUWA KUKABIDHIWA KWAO KUIONGOZA WIZARA HIYO YENYE MAJUKUMU MAZITO NA
INAYOTEGEMEWA NA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZAKE NI CHANGAMOTO
AMBAYO WANAPASWA KUIKABILI KWA KUDHIHIRISHA WELEDI NA UWEZO WAO KWA KUFANYA
KAZI KWA PAMOJA NA KWA KARIBU NDANI YA WIZARA NA KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA
NYINGINE.
DK. SHEIN ALIELEZA
MATUMAINI YAKE KUWA UONGOZI HUO MPYA WA WIZARA UTAENDELEA PIA KUFANYA KAZI KWA
KARIBU NA WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KATIKA KUTEKELEZA
MAJUKUMU YAKE KWA MAMBO YANAYOZIHUSU SERIKALI ZOTE MBILI.
RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AMEMPONGEZA WAZIRI SAADA NA
MANAIBU WAKE KWA UTEUZI HUO NA PIA KUWASHUKURU KWA KURIDHIA UTEUZI HUO KITENDO
AMBACHO ALIKIELEZA KUWA KINADHIHIRISHA DHAMIRA YAO YA KWELI YA KUWATUMIKIA
WANANCHI.
NAYE WAZIRI
WA FEDHA BIBI SAADA MKUYA SALUM ALIMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUWAPA FURSA YA
KUKUTANA NAE AMBAPO WAMEWEZA KUJIFUNZA MENGI KUTOKANA NA NAHASA ZAKE WAKATI WA
MAZUNGUMZO HAYO.
ALIONGEZA
KUWA UJIO WAKE NA TIMU YAKE UMELENGA SIO TU KUJITAMBULISHA BALI PIA
KUUHAKIKISHIA UONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWA WIZARA YAKE
ITAENDELEA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANA NA KWA KARIBU WAKATI WOTE.
WAZIRI SAADA
ALIBAINISHA KUWA ANATAMBUA KUWA WIZARA HIYO INASHUGHULIKIA PIA MASUALA YA
MUUNGANO HIVYO ATAHAKIKISHA KUWA KUNAKUWEPO NA USHIRIKIANO WA KARIBU NA
UTEKELEZAJI WA HARAKA WA MALENGO YALIYOWEKWA KWA MANUFA YA SERIKALI ZOTE MBILI.
MAZUNGUMZO
HAYO YALIHUDHURIWA PIA NA KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE,
KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK.
SERVACIUS LIKWELILE, KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR BWANA OMAR MUSSA, MKURUGENZI WA TAWI LA BENKI KUU YA TANZANIA,
ZANZIBAR BWANA NICODEMUS MBOJE NA MENEJA WA UTAWALA NA FEDHA WA TAWI HILO BWANA
MANSOUR ABDALLA.
No comments:
Post a Comment