tangazo

tangazo

Thursday, January 16, 2014

kesi inayowakabili viongozi wa HARAKATI YA Jumuiya NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR .


ZANZIBAR.

 

Mahkama kuu Vuga Mjini Zanzibar imeutaka upande wa mashtaka  kuwasilisha vielelezo na maelezo ya ushahidi vitakavyotumika  katika kesi inayowakabili viongozi wa  HARAKATI YA Jumuiya NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR .

 

Jaji wa Mahkama hiyo Fatma Hamid Mahmoud AMETOA OMBI HILO alipokuwa akiendesha kesi  INAYOWAKABILI VIONGOZI HAO katika Mahakam kuu Vuga Mjini Zanzibar .

 

JAJI HUYO pia AMEUTAKA UPANDE WA MASHTAKA kuwasilisha kwa maAndishi sababu za  kuzuiya dhamana ya  viongozi hao waliokaa RUMANDE  kwa MWAKA MMOJA SASA.

 

Hatua hiyo imeKUJA  baada ya mwendesha mashtaka wa Serikali Rashid Abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushaHidi wa kesi hiyo tayari vimekamilia hivyo  ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vieleLEzo vya mashahidi.

 

Kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa wa kesi hiyo Abdalla Juma  ameiomba mahkama KUPANGA tarehe ya kusikilizwa  KWA KESI hiyo NA vielelezo viwasilishwe mahkamani hapo kUTOKANA NA  ushahidi wa kesi hiyo KUkamilika.

 

Hata hivyo upande wa mashitaka haukuwa na pingamizi na na Ombi hilo na  umedai kuwa unaiachia mahkama kuamua.

 

Watuhumiwa KATIKA KESI HIYO  ni   AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH Farid Hadi Ahmed  mkaazi wa Mbuyuni,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH Mselem Ali Mselem  mkaazi wa Kwamtipura, USTADDH Mussa Juma Mussa  mkaazi wa Makadara 

Wengine ni  MAUSTADH Suleiman Juma Suleiman  mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma mkaazi wa Mwanakwerekwe ,KATIBU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR  AL-USTADH Abdallah Said mkaazi wa Misufini na Fikirini Majaliwa Fikirini.

 

Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali,  Uchochezi,Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa.

 

Kosa la nne liNAmkabili mshitakiwa namba nne AL-. NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR  AL-USTADH Azan Khalid ( mkaazi wa Mfenesini.

 

USTADH Azan Khalid HAMDAN anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa Kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

 

Vitendo hivyo vinadaiwa   kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 MWAKA 2013 katika maeneo  MBALI MBALI katika manispaa ya mji wa Zanzibar.

 

Jaji Fatma ameikhirisha Kesi hiyo na kutaka upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo  kabla ya  Januar 31 mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment