tangazo

tangazo

Monday, January 20, 2014

KONGAMANO LA WAISLAM

TEHRAN.
WASHIRIKI WA KONGAMANO LA 27 LA KIMATAIFA LA UMOJA WA KIISLAMU LILIMALIZA MJINI TEHRAN NCHINI IRAN WAMESISITIZWA KUEPUKA KHITILAFU ZA KISIASA ZINAZOPELEKEA KUZUSHA MGAWANYIKO KATI YA UMMA WA KIISLAMU.
KONGAMANO HILO LILILOZUNGUMZIA MADA 20 LIMELAANI JINAI ZA UTAWALA WA IZRAIL  DHIDI YA WAPHALESTINA, NAKUTOA WITO WAKUTEKELEZWA HAKI ZA KISHERIA ZA TAIFA LA PHALESTINA.
 HATA HIVYO WASHIRIKI WA KONGAMANO HIYO WAMEELEZEA UMUHIMU WAKUUNDWA TAIFA HURU LA PHALESTINA MJI MKU WAKE UKIWA BAYTUL-MUQADDAS SAMBAMBA NA KUREJEA WAKIMBIZI WA KIPHALESTINA.

KONGAMANO HILO LA KIMATAIFA LA UMOJA WA KIISLAMU, WASHIRIKI WAMESHAURI KULINDWA HESHIMA KATI YA WAISLAMU NA KUACHA NAKUEPUKWA MAMBO YENYE KHITILAFU KWA MAULAMA NA WATAALAMU SAMBAMBA NA KUTOVUNJIWA HESHIMA NA KUDHARAULIWA WANAWAZUONI WAKIISLAM. 

No comments:

Post a Comment