RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEKUTANA
NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI INSPEKTA JENERALI WA
POLISI ERNEST MANGU.
MKUU HUYO WA
JESHI LA POLISI ALIFIKA IKULU KUJITAMBULISHA BAADA YA KUTEULIWA HIVI KARIBU NA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUSHIKA
WADHIFA HUO.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMPONGEZA IGP MANGU KWA KUTEULIWA KUSHIKA WADHIFA
HUO NA KUMSHUKURU KWA KUKUBALI UTEUZI HUO AMBAO UNAMPA JUKUMU KUBWA LA KUONGOZA
JESHI HILO AMBAO WAJIBU WAKE WA KWANZA NI KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO.
DK SHEIN
ALIMUELEZA IGP MANGU KUWA JESHI LA POLISI ZANZIBAR LINASHIRIKI VYEMA KATIKA
KUHAMI UCHUMI WA ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA MAALUM ZA SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA KUKABILIANA NA MAGENDO YA KARAFUU NA PIA ULINZI
KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA HASA YA KITALII.
ALIONGEZA
KUWA ANAFARAJIKA KUONA KUWA KUNA UHUSIANO MZURI NA USHIRIKIANO WA KARIBU KATI
YA JESHI LA POLISI ZANZIBAR NA WANANCHI HALI AMBAYO IMESAIDIA KATIKA KUIMARISHA
ULINZI NA USALAMA NCHINI KUPITIA POLISI JAMII.
AMEFAFANUA
KUWA MFUMO WA POLISI JAMII UMESAIDIA KULETA UTULIVU KATIKA MITAA HIVYO
KUPUNGUZA VISA VYA UHALIFU KAMA VYA UVUNJAJI WA NYUMBA NA WIZI.
KWA HIVYO
ALISEMA KWA UJUMLA HALI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI NI SHWARI PAMOJA NA
KUBAINISHA KUWA YAPO MATUKIO YA HAPA NA PALE YA WIZI HASA KATIKA MAENEO YA
WATALII.
DK. SHEIN
AMEMWAMBIA IGP MANGU KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKUWA IKICHUKUA
HATUA KADHA WA KADHA KUIMARISHA USALAMA KATIKA MAENEO YENYE SHUGHULI ZA KITALII
LAKINI ALIBAINISHA KUWA JESHI LA POLISI HALINA BUDI KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA
KUUNGA MKONO HATUA HIZO.
AKIFAFANUA
ZAIDI, DK. SHEIN ALISEMA USALAMA KATIKA SEKTA YA UTALII NI KIPAUMBELE CHA
KWANZA KWA KUWA SEKTA HIYO, KWA MUJIBU WA MPANGO WA KUPUNGUZA UMASIKINI NA
KUKUZA UCHUMI ZANZIBAR-MKUZA, NDIO SEKTA KIONGOZI KATIKA UCHUMI AMBAYO
INAIPATIA ZANZIBAR ASILIMIA 80 YA FEDHA ZA KIGENI NA KUCHANGAIA ASLIMIA 27 YA
PATO LAKE.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO IGP MANGU AMBAYE ALIKUWA AMEFUATANA NA NAIBU INSPETA JENERALI
WA POLISI ABDULRAHMAN KANIKI NA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR CP HAMDANI OMAR
MAKAME ALIMUELEZA RAIS KUWA JESHI LAKE LIMEJIPANGA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE
IKIWEMO KUKABILIANA NA VITENDO VYOTE VYA KIHALIFU.
ALIELEZA
KUWA JESHI LAKE LINAJIIMARISHA ZAIDI KATIKA MASUALA YA UCHUNGUZI WA MATUKIO YA
KIHALIFU ZAIDI ILI KUZUIA VITENDO HIVYO KUFANYIKA KABLA HAVIJALETA ATHARI KWA
JAMII.
No comments:
Post a Comment