tangazo

tangazo

Sunday, January 19, 2014

makamo


WILAYA YA KISARAWE.

 

Chama cha wananchi cuf kimesema kuwa iwapo kitapewa mamlaka ya kuongoza dola, kitahakikisha kuwa kinaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Tanzania, ili kutoa fursa kwa wataalamu wa Itikadi tofauti za vyama vya siasa kushiriki katika serikali na kuwa kichocheo cha maendeleo.

 

Akizungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Msanga sokoni Wilaya ya Kisarawe,mkoaniwa pwani katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa mabadiliko ya kiuongozi yanahitajika katika kuwakomboa wananchi kiuchumi na kijamii.

 

amewashauri wanatanzania  kuachana na vyama vilivyopoteza muelekeo, na badala yake kukiunga mkono chama chenye dira ya kuwaletea maendeleo.

 

Amesema hatma ya maendeleo ya wananchi iko kwa wananchi wenyewe, na kwamba ndio wenye maamuzi ya kuchagua uongozi wanaoutaka kwa maendeleo yao na taifa kwa jumla.

 

 

Amesema ni jambo la kushangaza kuona Tanzania imeachwa nyuma kimaendeleo katika kipindi cha miaka 53 ya uhuru, huku nchi nyengine zilizokuwa hadhi sawa na Tanzania zikipiga hatua kubwa za maendeleo.

 

Amezitolea mfano baadhi ya nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kuwa ni pamoja Singapore na Malaysia, nchi ambazo zilikuwa maskini kuliko Tanzania, na kwamba Tanzania ina mengi ya kujifunzo kutoka nchi hizo.

 

“Singapore na Malaysia zilikuwa nchi maskini kuliko nchi yetu, lakini sasa zamepaa hadi dunia ya pili kuelekea ya kwanza kwa maendeleo. Hii imetokana na uongozi na mipango bora ya maendeleo waliyojiwekea”, alifafanua Maalim Seif.

 

Amefahamisha kuwa kitu cha kushangaza ni kuona Tanzania ina rasilimali nyingi zaidi kuliko nchi hizo lakini imedumaa kimaendeleo, jambo ambalo linapaswa Watanzania walitafakari kwa kina na kulitafutia ufumbuzi muafaka.

 

 

Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewaeleza wananchi kuhusu mafanikio yaliyopatikana Zanzibar tokea kuanzishwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

 

Amesema kuwa kuundwa kwa serikali hiyo kumetokana na maamuzi ya wananchi wengi wa Zanzibar, na kuwabeza wale wanaoubeza mfumo huo ambao pamoja na mambo mengine umerejesha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari.

 

Ameyataja mafanikio mengine ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuwa ni pamoja na kuongezwa kwa bei ya karafuu kutoka shilingi elfu tatu hadi elfu 15 kwa kilo moja, na  kupunguzwa kwa gharama za pembejeo za kilimo.

 

Mapema akizungumza katika mkutano huo, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi wa CUF Abdul Kambaya amesema kuwa bado Wilaya ya Kisarawe inakabiliwa na matatizo ya miundombinu ya barabara, elimu na afya.

 

Amewasisitiza  wananchi wa Wilaya ya kisarawe kubadilisha mfumo wa uongozi, ili kuwezesha rasilimali za nchi ziweze kutumika vizuri kwa maslahi ya wananchi wote.

 

Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kichama katika Wilaya hiyo na kufungua matawi ya CUF, pamoja na kukabidhi baiskeli ya matairi matatu kwa ndugu Khamis Salum mwenye ulemavu, ili iweze kumsaidia katika harakati zake za kimaisha.

No comments:

Post a Comment