SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUENDELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA SEKTA
YA AFYA NI SUALA INALOLIPA KIPAUMBELE KATIKA MIPANGO YAKE YA KUIMARISHA SEKTA
YA AFYA NCHINI.
RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA
HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA
SHIRIKA LA AFYA ULIMWENGUNI-WHO ZANZIBAR DK. PIERRE KAHOZI ALIYEMTEMBELEA
OFISINI KWAKE IKULU KWA AJILI YA KUMUAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA
KULITUMIKIA SHIRIKA HILO NCHINI.
AMESEMA
SERIKALI INATAMBUA CHANGAMOTO INAZOIKABILI KATIKA KUDUMISHA MAFANIKIO HAYO
YAKIWEMO VITA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA NA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO
LAKINI KURUDI NYUMA KATIKA MASUALA HAYO ITAKUWA NI KOSA KUBWA.
KWA HIYO
ALIMUELEZA DK. KAHOZI KUWA SERIKALI INAENDELEZA JITIHADA ZAKE ZA KUPAMBANA NA
MALARIA PAMOJA NA VITA DHIDI YA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO KWA KUCHUKUA HATUA
MBALIMBALI IKIWEMO KUONGEZA BAJETI YA SEKTA YA AFYA ILI KUENDELEZA VITA HIVYO.
AKITOLEA
MFANO WA VITA DHIDI YA MALARIA, DK SHEIN ALISEMA KUWA MAFANIKIO KUTOKA UWEPO WA
ASILIMIA 40 YA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUO HADI KUFIKIA CHINI YA ASILIMIA MOJA NI
MATOKEO YA JITIHADA ZA PAMOJA KATI YA SERIKALI NA WASHIRIKA WA MAENDELEO HIVYO
KUZIENZI JITIHADA HIZO NI KUIONDOA KABISA MALARIA NCHINI.
KWA UPANDE
WA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO ALIELEZA KUWA KUMEKUWEPO NA MAFANIKIO KUTOKA VIFO
476 MWAKA 2006 HADI VIFO 221 MWAKA 2013 KWA KILA MAMA WAJAWAZITO LAKI MOJA NA
JITIHADA ZAIDI ZINAFANYIKA ILI KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KATIKA SUALA HILO.
ALIBAINISHA
KUWA MBALI YA KUONGEZA BAJETI YA SEKTA YA AFYA LAKINI PIA SERIKALI YA MAPINDUZI
YA ZANZIBAR IMEBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WA AFYA ILI KUWAVUTIA KUBAKI NCHINI
KULITUMIKIA TAIFA BADALA YA KWENDA NJE AMBAPO KUSABABISHA UHABA WA WATUMISHI
HAO.
KATIKA
MAZUNGUMZO HAYO YALIYOHUDHURIWA PIA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA DK. SALEH
MOHAMED JIDAWI, DK. SHEIN ALISEMA KWA UPANDE MWINGINE SERIKALI IMEWEKA MKAZO
KATIKA KUFUNDISHA WATAALAMU ZAIDI WA SEKTA YA AFYA KWA KUWA HIVI SASA SEKTA
HIYO INAKABILIWA NA TATIZO LA UHABA WA WATUMISHI HUSUSAN KADA YA MADAKTARI.
AKIFAFANUA
ZAIDI ALIELEZA KUWA HATUA HIZO NI PAMOJA NA KUTOA MAFUNZO KWA KUSHIRIKIANA NA
CHUO KIKUU CHA TIBA HUKO CUBA, KUANZISHA SKULI YA UDAKTARI KATIKA CHUO KIKUU
CHA ZANZIBAR-SUZA NA KUPELEKA NJE WATUMISHI WA AFYA KUPATA MAFUNZO ZAIDI.
KWA UPANDE
WAKE DK. KAHOZI ALIIPONGEZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA MAFANIKIO
YAKE ILIYOYAPATA KATIKA SEKTA YA AFYA YAKIWEMO YA KUPIGA VITA UGONJWA WA
MALARIA NA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO AMBAPO ALIHIMIZA JITIHADA ZAIDI ZIFANYWE
KUHAKIKISHA KUWA MAFANIKIO HAYO YANAKUWA ENDELEVU.
KWA HIYO
ALITOA WITO KWA SERIKALI KUONGEZA ZAIDI BAJETI YA SEKTA YA AFYA KWA KUWA AFYA
NI SEKTA MUHIMU KWA SEKTA NYINGINE ZINAHITAJI WATUMISHI WENYE AFYA KUTEKELEZA
MAJUKUMU YAO.
ALIBAINISHA
KUWA KUONGEZWA BAJETI KATIKA SEKTA HIYO KITAKUWA KUVUTIO KWA WASHIRKA WA
MAENDELEO NAO KUONGEZA MISAADA YAO KATIKA SEKTA HIYO IKIWA NI KIELELEZO CHA
KUTHAMINI WAJIBU WA SERIKALI KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI WAKE.
No comments:
Post a Comment