MOGADISHU
MAREKANI IMEENDELEA KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI (DRONE) KUUA
WATU NCHINI SOMALIA LICHA YA MALALAMIKO YANAYOONGEZA YA KIMATAIFA DHIDI YA
MASHAMBULIZI HAYO YANAYOUA IDADI KUBWA YA RAIA WASIO NA HATIA KATIKA MAENEO
MBALIMBALI DUNIANI.
AFISA MMOJA WA JESHI LA MAREKANI AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LITAJWE
AMESEMA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA NCHI HIYO JANA JUMAPILI ZILISHAMBULIA
MSHUKIWA WA KUNDI LA AL SHABAB NCHINI SOMALIA.
HATA HIVYO AFISA HUYO WA JESHI LA MAREKANI HAKUTOA MAELEZO ZAIDI
KUHUSU MLENGWA NA IWAPO OPERESHENI HIYO ILIKUWA NA MAFANIKIO AU LA.
MAAFISA WA MAREKANI WANASEMA KUWA MLENGWA ALIKUWA AFISA WA NGAZI
ZA JU WA KUNDI LA AL SHABAB NA KWAMBA ALIKUWA AKIFUATILIWA NA MAREKANI KWA
MIAKA MINGI.
AFISA MWINGINE WA JESHI LA MAREKANI AMESEMA KUWA SHAMBULIZI HILO
LILIFANYIKA KARIBU NA ENEO LA BARAWE LILILOKO UMBALI WA MAILI 110 KUTOKA
MOGADISHU.
MWEZI OKTOBA MWAKA JANA MAKOMANDOO WA JESHI LA MAREKANI WALIFANYA
JARIBIO LA KUMTEJKA NYARA KIONGOZI WA AL SHABAB IKRIMA KATIKA MJI WA BARAWE
LAKINI OPERESHENI HIYO HAIKUFANIKIWA.
UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA BUREAU OF INVESTIGATIVE JOURNALISM (TBIJ)
YENYE MAKAO YAKE NCHINI UINGEREZA UNAONYESHA KUWA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA
MAREKANI ZIMEUWA KWA AKALI WATU 2,400 DUNIANI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO
TOKEA RAIS BARACK OBAMA ACHUKUE MADARAKANI NCHINI HUMO
No comments:
Post a Comment