RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN LEO
AMEWAAPISHA ND. AHMED KASSIM HAJI KUWA NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA
PILI WA RAIS NA BIBI RUKIA MOHAMED ISSA KUWA MJUMBE WA KAMISHENI YA UTUMISHI WA
UMMA NCHINI.
KUAPISHWA
KWA WATENDAJI HAO KUNAFUATIA UTEUZI WAO ULIOFANYIKA HIVI KARIBUNI AMBAPO
MHESHIMIWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIMTEUA PIA
DK. MOHAMED SEIF KHATIB KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR.
MIONGONI MWA
VIONGOZI WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO YA KUAPISHWA NI PAMOJA NA MAKAMU WA PILI WA
RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI, JAJI MKUU WA ZANZIBAR MHESHIMIWA OMAR MAKUNGU, SPIKA
WA BARAZA LA WAWAKILISHI MHESHIMIWA PANDU AMEIR KIFICHO, MUFTI MKUU WA ZANZIBAR
SHEIKH OMAR SALEH KABI, KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE,
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MJI WA ZANZIBAR MHESHIMIWA KHATIB ABDULRAHMAN KHATIB
NA MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ABDALLA MWINYI KHAMIS.
No comments:
Post a Comment