ZANZIBAR
WAUMINI
WA DINI YA KIISLAM NCHINI WAMETAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WANAPOFUNGIWA
BIDHAA MBALI MBALI KWA KUTUMIA MAGAZETI AMBAYO MARA NYINGINE HUWA NA MAANDISHI
MATAKATIFU YA QUR-AN.
WITO
HUO UMETOLEWA LEO NA MUFTI MKUU WA ZANZIBAR SAMAHATU SHEKHE SALEH OMAR KAABI
ALIPOKUTANA NA BAADHI YA VIJANA OFISINI KWAKE WALIOMPELEKEA MAGAZETI AMBAYO
HUTUMIWA NA WAFANYA BIASHARA KWA AJILI YA KUFUNGIA BIDHAA MBALI MBALI HUKU
BAADHI YA MAGAZETI HAYO YAKIWA NA AYA ZA QUR-AN NA HADITHI ZA MTUME.
KWA
MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU WA MUFTI WA ZANZIBAR FADHILATU SHEKHE
FADHILI SORAGA AMESEMA MUFTI MKUU AMELAANI VIKALI MTINDO HUO ULIOZUKA NA ZAIDI
KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI.
AMESEMA
WAUMINI WOTE WANAPASWA KUHESHIMU MAANDISHI HAYO MATAKATIFU NA NI MAKOSA MAKUBWA
KWA MAANDISHI HAYO KUTUMIKA KUFUNGIA BIDHAA.
HATA HIVYO OFISI YA MUFTI ZANZIBAR IMEWATAKA WAINGIZAJI
WOTE WA MAGAZETI YA KUFUNGIA BIDHAA KUTOKA NCHI ZA KIARABU,WANUNUZI NA WALE
WANAOFUNGIA NA WALE WANAOFUNGIA BIDHAA KWA MAGAZETI HAYO KUHAKIKISHA KWAMBA AYA
ZA QUR-AN TAKATIFU HAZITUMIKI NA HADITHI ZA MTUME (S.A.W) HAZITUMIKI KWA
MALENGO HAYO.
No comments:
Post a Comment