zanzibar.
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA INAKUSUDIA
KULIJENGA UPYA SOKO KUU LA DARAJANI MJINI ZANZIBAR ILI KUONDOSHA USUMBUFU
WANAUPATA WAFANYABIASHARA WA SOKO HILO.
HAYO YAMEELEZWA NA Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NDUGU Haji Omar Kheir WAKATI AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO CHUKWANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AMEFAFANUA KUWA SEREKALI INAFAHAMU SUALA LAKUWEPO VIPENU NA UCHAKAVU WA BAADHI YA SEHEMU ZA SOKO HILO HIVYO IMEAMUA KULIJENGA UPYA KWA NJIA YAKUTANGAZA TENDA
AIDHA WAZIRI HUYO AMEBAINISHA KUWA SEREKALI IMESHAANDAA MICHORO YA UJENZI WA SOKO HILO NA KILICHOBAKI NI KWA MAMLAKA YA MJI MKONGWE WA ZANZIBAR KUIKUBALI NAKUTOA MAELEKEZO YATAKAYOZINGATIA KUENDELEZWA KWA URITHI WA MJI HUO WAKIMATAIFA.
No comments:
Post a Comment