PEMBA.
MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA DADI
FAKI DADI AMEWATAKA WALIMU WAKUU KATIKA WILAYA YA MICHEWENI KUANDAA MAZINGIRA
YATAKAYO WAFANYA WANAFUNZI KUONDOA NA
DHANA KWAMBA MASOMO YA SAYANSI NI MAGUMU .
KAULI HIYO AMEITOA WAKATI AKIZUNGUMZA NA WALIMU WAKUU NA WENYEVITI WA KAMATI ZA SKULI ZA WILAYA
HIYO KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SKULI YA WINGWI .
AMESEMA KUWA DHANA HIYO AMBAYO IMEJENGEKA MIONGONI MWA WANAFUNZI INAPASWA
KUONDOSHWA ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI .
AMESEMA KUWA MOJA YA MIKAKATI HIYO NI PAMOJA NA KUANDAA
WANAFUNZI KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI WAKIWA SKULI ZA MSINGI
HALI AMBAYO ITAWAJENGA UWEZO WA KUKABILIANA NA MASOMO HAYO .
NAO WASHIRIKI WA KIKAO HICHO WAMEIOMBA SERIKALI YA MKOA KUANDAA ZIARA
MAALUMU YA KUTEMBELEA SKULI ZOTE NA KUZUNGUMZA NA WAZAZI ILI KUWAHAMISHA
KUCHANGIA KAMBI ZA WANAFUNZI ZILIZOANZISHWA KWA LENGO LA KUWANDAA WANAFUNZI .
WAMESEMA KUWA LICHA YA WALIMU NA
KAMATI ZA SKULI KUWA NA MALENGO MAZURI YA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA
WILAYA HIYO BADO JUHUDI ZAO ZIMEKUWA ZIKIVUNJWA NA WAZAZI AMBAO WAMEKUWA WAGUMU
KUCHANGIA ILI KUENDELEZA KAMBI ZA MASOMO .
No comments:
Post a Comment