ZANZIBAR.
Jumla ya skuli 21 za
sekondari zimejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya ZanziBar kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (Badea)
HAYO YAMEELEZWA Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Amali ZANZIBAR Zahra Ali Hamad wakati AJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA
BARAZA LA WAWAKILISHI katika KIKAO CHA
BARAZA HILO KINACHOENDELEA HUKO Chukwani
NJE KIDOGO YA MJI WA ZANZIBAR.
Bi. Zahra
amemuhakikishia Mwakilishi huyo kwamba mpango wa kujenga skuli ya ghorofa
katika eneo la skuli hiyo upo kutokana na kubainika kuwepo kwa idadi kubwa ya
wanafunzi katika mitaa ya karibu na skuli hiyo.
AMEsema kuwa
LICHA YA utekelezaji wa mpango huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kwa kushirikiana na mfuko wa OPEC inakusudia kujenga skuli kumi 10 za
ghorofa ambapo mradi huo ulichelewa kuanza kutokana na kutokamilika
taratibu za kisheria kuhusu makubaliano ya mkopo.
Wakati huo huo
Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati inakusudia kumaliza
tatizo la upatikanaji wa huduma Ya maji ifikapo mwaka 2017 kwa Wananchi
wa Mji mkogwe na Ng’ambu.
Hayo yameelezwa na
Naibu Waziri wa wizara hiyo Haji Mwadini Makame wakati
akijibu MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR.
Amesema kuwa
wanakusudia kumaliza tatizo kwa kuimarisha huduma hiyo kwa kuimarisha miundo
mbinu ikiwemo kubadilisha Mabomba ya zamani ambayo yamechoka na
kushindwa kuhimili ongezeko kubwa la wahamiaji.
Aidha
aMEBAINISHA kuwa hali ya upatikanaji wa
maji katika Mkoa wa Mjini inaendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kuna
baadhi ya maeneo yanapata Maji kwa muda mrefu na mengine yanapata maji kwa mgao
hasUSAN wakati wa kiangazi na maeneo machache hukosa kabisa.
AMESema KUWA kupitia Mamlaka ya maji wamekuwa
wakifanya juhudi kutafuta ufumbuzi wa suala hilo ikiwa ni pamoja na
uchimbaji wa Visima vipya katika maeneo mbali
mbali.