PEMBA.
MAKAMO MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF TAIFA AL-HAJJ JUMA
DUNI HAJJI AMESEMA KUWA CHAMA HICHO
KIMEKUWA NA UTARATIBU WA KUWAOMBEA DUA WANACHAMA WAKE WALIOTANGULIA
MBELE YA HAKI KILA MWAKA, KWA LENGO LA KUKUMBUKA MCHANGO WALIOUTOA.
KIONGOZI
HUYO AMEYASEMA HAYO KATIKA DUA MAALUM YAKUWAOMBEA WANACHAMA WA CUF
WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI ILIOFANYIKA
KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA CHACHANI CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA.
AMEONGEZA KUWA WALICHOKIFANYA WANACHAMA HAO
HADI KUPOTEZA MAISHA, KIMELETA FAIDA KUBWA
NA MCHANGO WAO, HAUTOSAULIKA .
DUA HIYO PIA IMEHUDHURIWA NA MWAKILISHI WA
JIMBO LA MJI MKONGWE ISMAIL JUSSA LADU, MWAKILISHI W AJIMBO LA CHAKE
CHAKE ,OMARI ALI SHEHE NA WENYEVITI NA MAKATIBU WA CUF WA WILAYA NNE ZA PEMBA.
DUA
HIYO NI MAALUMU KWA AJILI YAKUWAOMBEA WANACHAMA WA CHAMA CHA WANANCHI
CUF WALIFARIKI MAPEMA MWAKA 2001.
KUFUATIA HALI HIYO, CHAMA CHA WANANCHI CUF,
KIMEAMUA KUPEPERUSHA BENDERA ZAKE NUSU MLINGOTI NCHI NZIMA KUANZIA JANA.
No comments:
Post a Comment