WILAYA
YA MJINI.
WAUMINI
WA DINI YAKIISLAM KOTE NCHINI WAMETAKIWA KUJITOLEA KWA HALI NA MALI KUWASAIDIA
WATOTO YATIMA AMBAO WAKO KATIKA HALI NGUMU YA MAISHA.
NASAHA HIZO ZIMETOLEWA NA UKHTI BIMKUBWA ABDI NASSIR
WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM KATIKA MAHFAL YAKUKABIDHI MISADA YA WATOTO YATIMA
KATIKA UKUMBI WA SKULI YA SEKONDARI YAKIISLAM YA AL-FALAH ILIYOKO MOMBASA
WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
HATA HIVYO UKHTI BIMKUBWA AMESISITIZA HAJA KWA WAISLAM
KUTENGA FUNGU MAALUM KWA AJILI YA WATOTO HAO ILI KUPATA RADHI KUTOKA KWA MOLA
WAO.
KWA UPANDE WAKE NAIBU AMIRA WA KAMATI MAALUM YAKUSHUGHULIKIA WATOTO YATIMA UKHTI
RUKIA ALI MASHEKO AMESEMA KUWA LENGO KUU LA MFUKO WAKUWAPA MISAADA HIYO WATOTO
YATIMA NIKUWAPUNGUZIA UGUMU WA MAISHA NAKUZIPUNGUZIA MZIGO FAMILIA
ZILIZOCHUKUWA JUKUMU LAKUWALEA WATOTO HAO.
JUMLA YA WATOTO YATIMA 131 WA UNGUJA NA PEMBA WANAPATIWA
VIFAA MBALI MBALI VYA SKULI NA CHUO CHA AL-FALAH ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment