ZANZIBAR.
MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar M Maalim
Seif Sharif Hamad, amewasisitiza wananchi kufuata taratibu na maelekezo ya
hospitali, ili kuwawekea wagonjwa mazingira bora.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika hafla ya
ufunguzi wa kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) cha hospitali kuu ya Mnazi
Mmoja, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51 na Mapinduzi ya
Zanzibar.
Amesema KUWA wagonjwa hasUSAN wanaotibiwa katika
wodi ya wagonjwa mahututi wanahitaji utulivu na uangalizi maalum, hivyo hakuna
budi kwa wananchi kwa watendaji wa hospitali na wananchi kuwawekea mazingira
bora kwa ajili ya matibabu yao.
Sambamba na hilo Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar amewahimiza wafanyakazi wa hospitali kuwa wapole na wavumilivu wakati
wote, ili kuwapa matumaini wagonjwa na wananchi wanaofika hospitali kwa ajili
ya kupatiwa huduma.
Amesema kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu
kwa wafanyakazi wa hospitali kutokuwa na lugha nzuri wakati wanapowahudumia
wagonjwa, jambo ambalo linakiuka maadili ya taaluma ya afya.
Amesema wakati umefika kwa wafanyakazi hao
kubadilika ili kulinda heshima ya taaluma hiyo na kujenga matumaini mapya kwa
wagonjwa wanaofika hospitali.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa
Afya Rashid Seif Suleiman, amesema kuwa serikali inajitahidi kupata vifaa vya
kisasa vya uchunguzi, ili kuwawezesha madaktari kufanya kazi zao kwa uhakika.
Amesema katika kuimarisha sekta ya afya, Wizara
hiyo ina mpango wa kupata dawa kwa ajili ya matumizi ya Zanzibar bila ya kupita
muda wake wa matumizi, sambamba na kujenga wodi mpya ya akinamama wanaokwenda
kujifungua katika hospitali hiyo.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Mohamed
Saleh Jidawi, amesema lengo la kujengwa kwa wodi hiyo mpya ni pamoja na kuinua
afya za wananchi pamoja na kuokoa maisha yao.
No comments:
Post a Comment