tangazo

tangazo

Tuesday, January 27, 2015

SERIKALI YA TANZANIA IMEKUSUDIA KUPUNGUZA MSONGAMANO KATIKA JIJI LA DAR-ES-SALAAM



DAR-ES-SALAAM.

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMESEMA KUWA IMEKUSUDIA  KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI  KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KWAKUJENGA
BARABARA SITA AMBAZO UJENZI WAKE UTASIMAMIWA NA TANROADS.

HAYO YAMEELEZWA NA WAZIRI
WA UJENZI DKT.JOHN POMBE MAGUFULI WAKATI  AKIWEKA JIWE LA
MSINGI KUASHIRIA UZINDUZI RASMI WA UJENZI WA BARABARA HIZO.
 
AMESEMA  KUWA BARABARA HIZO ZINAJENGA KWA UFADHILI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA
ASILIMIA 100 NA LENGO KUBWA LA MRADI HUO NI KUPUNGUZA MSONGAMANO NDANI YA JIJI”.


HATA HIVYO WAZIRI MAGUFULI AMEBAINISHA KUWA UJENZI HUO UNATARAJIWA KUGHARIMU SHILINGI TRILIONI MOJA AMBAPO LENGO BARABARA HIZO NI  KUPUNGUZA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI  KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MJINI DAR ES
SAALAM.



KWA UPANDE WAKE MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM  SAID MECKY SADICK AMEWATAKA WANANCHI WA DAR ES
SALAAM KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA SERIKALI NA WAKANDARASI WATAKAPOOMBWA
KUSOGEA  NJE YA BARABARA ILI KUFANIKISHA
UJENZI HUO.



NAYE MTENDAJI  MKUU WAKALA WA USIMAMIZI
WA BARABARA (TANROADS) MHANDISI  PATRICK
MFUGALE AMEZITAJA BARABARA ZINAZOTARAJIWA KUANZA KUJENGWA KATIKA MRADI WA
KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA JIJINI LA DAR ES SALAAM KUWA NI PAMOJA NA UBUNGO MSEWE
HADI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM YENYE UREFU WA KILOMITA 2.6, UBUNGO EXTERNO
HADI KILUNGULE KILOMITA 3, NA KIGOGO HADI TABATA DAMPO KILOMITA 1.6.


No comments:

Post a Comment