DAR-ES-SALAAM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kutoka chama hicho KUoneshA mfano
kwa uongozi bora katika kuwatumikia wananchi na kukitangaza vyema chama hicho.
Maalim Seif aMEYAsema hayo leo KATIKA UKUMBI WA Makao
Makuu ya CUF Buguruni MJINI DAR-ES-SALAAM wakati akizungumza na viongozi wa
Serikali za mitaa kutoka CUF walioshinda katika uchaguzi wa mitaa, vijiji na
vitongoji uliofanyika mWISHONI MWA MWAKA JANA.
AMEsema KUWA wakati wa kampeni za uchaguzi wagombea wote
walijinadi kwa wananchi na walitoa ahadi mbali mbali, hivyo ni jukumu lao
kuzitekeleza kwa ufanisi mkubwa.
Mapema akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Tandale Kwatumbo kwa ajili ya kuwashukuru wana CUF na wananchi, Maalim Seif aMEsema
KUWA ni dhahiri KUWA matokeo mazuri ya wapinzani yalitokana na uamuzi wa vyama
vinne vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kuunganisha nguvu ZAO.
AMEsema KUWA katika uchaguzi huo CUF pamoja na vyama
vinavyounda UKAWA vilisimama imara kuhakikisha wananchi wenye sifa za kuwa
wapiga kura katika maeneo HUSIKA ndio wanaopiga kura na walioshinda ndio
wanaotangazwa.
Katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi
uliopita katika Kata ya Tandale, CUF kilishinda mitaa mitatu kati ya sita,
ambapo mtaa mmoja hadi sasa matokeo yake yamekumbwa na utata.
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa wa Kwatumbo, Mohammed Kassim alisema KUWA ushindi huo
unatokana na umakini wa wana CUF KATIKA kuhakikisha wanalina ushindi wao.
Hata hivyo aliwataka wanachama wa CUF na wananchi wa
Tandale KUTOtoshekA na wasijisahau kwa ushindi huo NA BADALA YAKE KUJIIMARISHA
zaidi na kuhakikisha wote wanajiandikisha katika daftari laKUPIGIA kura, ili
washiriki katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba MWAKA HUU.
Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika MWISHONI
MWA MWAKA JANA CUF ilipata viti 19 katika Wilaya ya Ilala, viti 34 Temeke na
viti 20 Kinondoni.
No comments:
Post a Comment