WILAYA YA MJINI.
Wananchi wa shehia ya kikwajuni welesi
wamelalamikia tatizo la ukosefu wa huduma ya maji safi na salama katika eneo
lao NAKUPELEKEA KUPATA usumbufu wa kufuata huduma hiyo katika maeneo ya jirani.
Wakizungumza na Adhana fm radio mmoja wa
wananchi hao Bi Asia Nassoro amesema kuwa kwa kipindi kirefu sasa
huduma hiyo imekosekana na kulazimika kununuwa maji ambayo si salama
kwa afya zao.
AmefahamishaKUWA licha ya kuwa serikali inachukuwa jitihada
mbalimbali za kuhakikisha kuwa wananchi wa visiwa vya unguja na pemba
wanapata maendeleo bila ya ubaguzi wamekuwa wakikosa fursa hiyo ya
kunufaika na matunda ya mapinduzi ya mwaka 1964.
Kwa upande wake afisa uhusiano Mamlaka ya Maji
Zanzibar (ZAWA) Zahoro SUleyman amesema KUWA tatizo la ukosefu wa huduma
ya maji safi na salama limechangiwa na uchakavu wa miundo mbinu na matumizi
mabaya ya wananchi.
Aidha amesema kuwa mamlaka ya maji kwa
kushirikiana na wadau husika wana mpango wa kuanzisha mradi wa kuwapatia
huduma ya maji wananchi wa maeneo ya MJI MKONGWE na vitongoji vyake kwa lengo la kuondoa
usumbufu.
Sambamba na hayo amefahamisha kuwa mradi
huo utaweza kuengeza kiwango cha upatikanaji wa maji safi.
AMEWATAKA
wananchi KUWA na utamaduni wa kulinda na kutunza vyanzo vya maji
ili waweze kunufaika na huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment