PARIS.
Mwanaharakati
wa Kiislamu nchini Ufaransa SHEIKH Aboubakar ALhaj Umar ameWATA Waislamu
wanaoishi katIka nchi za Magharibi
KUPANGA mIkakati madhubuti YAkuimarisha mshikamano wakiwa katika maeneo
mbalimbali barani Ulaya.
MWANAHARAKATI HUYO AMBAYE NI Naibu Mkuu wa Muungano wa
Taasisi za Kiislamu nchini Ufaransa amesema kuwa, hakuna shaka kuwa utawala wa
Israel uko mbioni kufanya njama za kutaka kUYATUMIA matukio ya mashambulio ya
kigaidi yaliyotokea Ufaransa kwa lengo la kujisafisha na kuichafua taswira ya
Harakati ya Hamas na wananchi wa PHalestina katika ANGA ZAkimataifa.
ameongeza
kuwa, licha ya hivi sasa wananchi wa Syria na Iraq kukabiliwa na mashambulio ya
makundi ya kigaidi wananchi wa PHalestina kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa
wakikabiliwa na vitendo vya kigaidi vya kiserikali vya utawala ghasibu wa
Israel.
Sheikh
Aboubakar amebainisha kuwa, ugaidi hauna dini na kusisitiza kwamba
vitendo vya kigaidi viKIPINGANA kikamilifu na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Kiongozi huyo wa Kiislamu amesema kuwa, pamoja
na kuwepo uhuru wa kujieleza, lakini uchapishwaji wa vikatuni na vibonzo vinavyomvunjia
heshima Mtume Muhammad saw na matukufu ya Kiislamu, ni mambo yasiyokubalika.
No comments:
Post a Comment