ZANZIBAR.
JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA WA CUF TAIFA IMEWATAKA
MASHEHA WOTE NCHINI KUTENDA HAKI
NAKUTIMIZA WAJIBU WAO KAMA WALIVYO WATUMISHI WA UMMA.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA KHABARI KATIKA UKUMBI WA
OFISI YA MAKAO MAKUU YA CUF VUGA MJINI ZANZIBAR MWENYEKITI WA JUMUIYA YA VIJANA
WA CUF TAIFA NDUGU HAMIDU BOBALI AMEKEMEA TABIA YA MASHEHA KUWAZUIA VIJANA WA
ZANZIBAR KUPATA VITAMBULISHO VYA MZANZIBARI MKAAZI NA VYAKUPIGIA KURA KUTOKANA
NA SABABU ZAKISIASA.
AIDHA MWENYEKITI HUYO AMEBAINISHA KUWA KUMEKUWA NA
MALALAMIKO KUTOKA KATIKA WILAYA NA MAJIMBO YOTE KUWA MASHEHA WAMEKUWA NI
KIKWAZO CHA VIJANA WALIOTIMIZA UMRI WAKUANDIKISHWA KUTOANDIKISHWA KWASABABU
ZAKISIASA.
HATA HIVYO KIONGOZI HUYO AMESEMA KUWA JUMUIYA YA UMOJA WA
VIJANA YA CUF TAIFA HAIKO TAYARI KUVUMILIA AINA YOYOTE YA HILA ZA MASHEHA DHIDI
YA VIJANA WAKIZANZIBARI NA WAZANZIBARI WOTE KWA JUMLA NA HAITOKWENDA MAHAKAMANI
NA KATIKA CHOMBO CHOCHOTE KUWASILISHA MALALAMIKO YAO KWA MADAI KUWA DALILI ZOTE
ZINAONYESHA KUWA KATIKA VYOMBO HIVYO HAKUNA HAKI YOYOTE ITAKAYOPATIKANA NA
BADALA YAKE ITAWAHAMASISHA VIJANA ILI KUHAKIKISHA WANAPATA HAKI ZAO ZA MSINGI.
JUMUIYA HIYO IMEONGEZA INAFAHAMU KWAMBA BAADHI YA
VIONGOZI WAKUBWA SEREKALI WAKO MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA KUWA KILA
MAZANZIBARI ANAYESHABIKIA CHAMA CHA WANANCHI CUF ANANYIMWA HAKI ZAKE ZA MSINGI.
TAARIFA HIYO YA UMOJA WA VIJANA WA CUF IMEMTAKA WAZIRI WA
NCHI AFISI YA RAIS NA IDARA MAALUM ZA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAJJI
OMAR KHERI KUACHA KUWATISHA VIJANA WA TUMBATU WANAOJIUNGA NA CUF.
MWENYEKITI HUYO AMETOA WITO KWA VIJANA WAKIZANZIBARI
AMBAO WAMEJIANDIKISHA KUPATA VITAMBULISHO VYA MZANZIBARI MKAAZI , VYAKUPIGIA
KURA NA VYA MTANZANIA KWENDA KATIKA VITUO VYA WILAYA ZAO KUCHUKUWA VITAMBULISHO
HIVYO.
AMEFAFANUA LICHA YA MUITIKIO MDOGO WA VIJANA KWENDA
KUCHUKUWA VITAMBULISHO VYAKUPIGIA KURA HIVI SASA VINATOLEWA KATIKA WILAYA ZOTE
ZA ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment