WILAYA YA KASKAZINI “ B.
MBUNGE WA JIMBO LA KITOPE BALOZI SEIF ALI IDDI AMESEMA KUWA LICHA YA JUHUDI
ZINAZOCHUKULIWA NA VIONGOZI KATIKA KUCHANGIA NGUVU ZA KUKABILIANA NA MATATIZO
MBALI MBALI YANAYOWAKABILI WANANCHI KATIKA MAENEO YAO BADO JUKUMU HILO
LITAENDELEA KUBAKIA MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE.
BALOZI SEIF AMBAE PIA NI MAKAMU WA
PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIKABIDHI MABOMBA 250 YA
KUSAMBAZIA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA KATIKA KITUO CHA KILIMO
KILOMBERO WILAYA YA KASKAZINI “ B “ MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
AMESEMA KUWA VIONGOZI NA SERIKALI
KUU HUHAMASIKA NA KUSHAWISHIKA ZAIDI KUSAIDIA HATA UWEZESHAJI NA HATA
VIFAA KWENYE MIRADI YA JAMII BAADA YA KUONA NGUVU ZA WANANCHI ZIMEANZA AU
KUIENDELEZWA KATIKA KUJIKOMBOA NA UMASKINI AU KUJITAFUTIA MAENDELEO YAO.
MABOMBA HAYO YALIYOGHARIMU JUMLA YA SHILINGI MILIONI 17,000,000/- NUSU YA
GHARAMA YA FEDHA HIZO IMETOKANA NA MFUKO WA JIMBO { CDF } NA NUSU ILIYOBAKIA
IMETOLEWA NA MBUNGE HUYO WA JIMBO LA KITOPE.
BALOZI SEIF PIA ALISHIRIKI KAZI YA UCHIMBAJI MTARO WA ULAZAJI WA BOMBA HIZO
UNAOANZIA KWENYE KISIMA KILICHOCHIMBWA KWA AJILI YA MRADI HUO WA USAMBAZAJI
MAJI AMBACHO KIMESHAKALIMIKA ULIOKWENDA SAMBAMBA NA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA
UMEME KATIKA KISIMA HICHO.
ALIWAPONGEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA KILOMBERO KWA KAZI KUBWA WANAYOENDELEA
KUIFANYA YA KUJIONDOSHEA MATATIZO YANAYOWAKABILI IKIWEMO KUSHIRIKI KATIKA KAZI
ZA USAMBAZAJI WA HUDUMA ZA MAJI SAFI.
BALOZI SEIF ALISEMA HUDUMA ZA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NI ZAO HIVYO LAZIMA
WAHAKIKISHE WANASHIRIKI KWA NGUVU ZAO ZOTE KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
KAMA HIZO ZA JAMII.
MAPEMA DIWANI WA WADI YA UPENJA BIBI ASHA ABDULLA MUSSA
AKIPOKEA MCHANGO WA MABOMBA HAYO YA USAMBAZAJI MAJI SAFI KATIKA KIJIJI
CHA KILOMBERO ALIMPONGEZA MBUNGE HUYO WA JIMBO LA KITOPE KWA MOYO WAKE WA
KUSAIDIA KUONDOSHA MATATIZO YANAYOWAKABILI WANANCHI WA JIMBO LAKE.
AKITOA SHUKRANI KWA NIABA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA KILOMBERO
MSIMAMIZI WA KAMATI YA MRADI WA MAJI YA KIJIJI HICHO BWANA MOH’D HAJI
FAKI ALIMUHAKIKISHIA MBUNGE HUYO WA JIMBO LA KITOPE KWAMBA WANANCHI WA KIJIJI
HICHO WAKO TAYARI MUDA WOWOTE KUSHIRIKI KATIKA KAZI ZA MAENDELEO WAKATI
WATAPOTAKIWA KUFANYA HIVYO.
ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 20,000,000/- ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE WA JIMBO LA
KITOPE BALOZI SEIF ALI IDDI ZIMETUMIKA KATIKA UJENZI WA KISIMA CHA MAJI
YA KILOMBERO KWA LENGO LA KUWAONDOSHEA USUMBUFU WA MIAKA MINGI WA HUDUMA ZA
UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA SALAMA WANANCHI WA KIJIJI HICHO.
No comments:
Post a Comment