ZANZIBAR.
Wadau
Wa Radio Adhana Kitaaluma Wameupongeza Uongozi Wa Radio Adhana Kwa Juhudi Zake
Katika Kuiendeleza KITUO HIKI Baada Ya
Kuzorota Chini Ya Wamiliki Wa Awali.
Wakizungumza
Katika Kikao Cha Pamoja Na Uongozi Wa Radio Wadau Hao Kutoka Jumuiya Ya
Istiqama TANZANIA TAWI LA ZANZIBAR Baada
Ya Kufanya Ukaguzi Na Kuisikia Ripoti Ya Kazi Za Radio Wametoa Njia Mbali Mbali
Za Kuiwezesha Radio Kujiendesha Kimapato.
Mapema
Mwenyekiti Wa Bodi YA RADIO ADHANA ShEIKH Salum Mohd Abdusalam Amewataka
Wajumbe Hao Kuangalia Namna Ya Kuisaidia Radio Adhana Ili Iweze
Kuendelea.Sambamba Na Kutoa Mapendekezo Ya Majina Ya Watu Ambao Watafaa
Kuingizwa Katika Bodi Ya Uongozi Wa Radio.
Akitoa
Taarifa Ya Kazi Za Radio Adhana Mkurugenzi Wa KITUO HIKI AL-USTADH Munir Ali Muhsin Ameelezea Mafanikio Na
Changamoto Mbali Mbali Zinazoikabili Radio ADHANA Katika KURUSHA Matangazo Yake
Ya Kila Siku.
Amesema
KUWA Ili KITUO HIKI KIWEZE Kuendelea
VIZURI Waislam Na Wasikilizaji
Wake Wana Wajibu Wa Kuisaidia Kwa Njia Mbali Mbali Ikiwa Ni Pamoja Na
Kuipatia Matangazo YA BIASHARA.
Uongozi
Wa Radio Adhana Umefanya Kikao Hicho Katika Ukumbi Wa Wa Radio Adhana Kwa
Kufanya Tathmini Ya Kazi Za Radio Kwa Mwaka Jana Wa 2014
Pamoja Na Kuwaalika Wadau Wa Radio Katika Mambo Ya Taaluma Kwa Lengo La Kupata
Ushauri Ambapo Jumla Ya Wajumbe Saba Walihudhuria.
No comments:
Post a Comment