zanzibar.
wazazi na walezi nchini wamempongeza rais wa zanzibar
dr ali mohd shein kutokana na kuondoa uchangiaji wa fedha kwa wanafunzi wa
skuli za msingi.
wakizungumza na adhana fm kwa nyakati tofauti wazazi
hao wamesema kuwa hatua hiyo itawatia nguvu wazazi kuwapeleka maskulini kwa
wingi watoto wao.
aidha wananchi hao wamebainisha kuwa wazazi wengi
wamekuwa wakilalamikia kuongezeka
michango mingi ya skuli nakupelekea baadhi ya wanafunzi wa hali za chini
kusimamishwa kuhudhuria maskulini kutokana nakutolipa ada jambo ambalo
linarejesha nyuma maendeleo ya elimu kwa watoto wao.
hata hivyo wazazi hao wameishauri serekali ya
mapinduzi ya zanzibar kulisimamia suala hilo kwa kuhakikisha kuwa viongozi na
watendaji hawakiuki agizo hilo la rais.
No comments:
Post a Comment