ZANZIBAR.
wanasiasa na wasomi NCHINI wameWAtaka wananchi kuPaNGA
mikakati muhimu ya maendeleo na kuacha fikra mgando zinazoathiri maendeleo ya
nchi yao.
WAKIZUNGUMZA NA ADHANA FM RADIO Wasomi na wanasiasa
hao WAmesema KUWA Zanzibar imepiga hatua kubwa za maendeleo kiuchumi, kijamii
na kisiasa AMBAPO zinaweza kuendelezwa au kuharibiwa na Wazanzibari wenyewe
iwapo wataWEKA MBELE tofauti zao za kihistoria zinazohusiana na mapinduzi.
KWA UPANDE WAKE Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria cha
Chuo Kikuu cha Zanzibar, Ali Uki aMEsema KUWA LICHA YA Zanzibar KUPIGA hatua
katika ujenzi wa miundombinu, huduma za kijamii, sheria, kilimo na maendeleo ya
kisiasa kudumisha amani ndilo jambo la msingi.
AMEBAINISHA KUWA TOKEA kuanza KWA mfumo wa vyama
vingi mwaka 1992, Zanzibar imekuwa ikijitahidi kuhimili misukosuko mbalimbali
ya kisiasa ukiwamo upinzani mkali KATI ya CCM na CUF uliosababisha kuundwa kwa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
LICHA YA mafanikio hayo, MUHADHIRI HUYO AMEELEZEA haja
ya kufanyWa mkutano wa kitaifa wa kukubaliana kiwango cha sera za kufuatwa kutoka
katika kila chama kUTOKANA na SEREKALI HIYO KUTUMIA sera za CCM PEKEE.
AIDHA UKI AMESHAURI KUWA Iwapo itaonekana KUWA HILO
NI tatizo katika mwaka huu wenye changamoto za Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu,
kila chama kinaweza kukaa katika kamati zake na wataalamu na kuamua kuhusu
kujumuisha sera zao ili kujenga mustakabali bora wa kisiasa Zanzibar.
KWA UPANDE WAKE Mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema), Tundu Lissu aMEsema KUWA mustakabali wa Muungano kati ya Zanzibar na
Tanganyika upo mikononi mwa wananchi wote na kwamba Kura ya Maoni ya Katiba
inaweza kuamua hatima yake.
No comments:
Post a Comment