ZANZIBAR.
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR
ALI JUMA SHAMUHUNA AMEWASHAURI WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI KUTUMIA ELIMU NA
UJUZI WANAOPATA KUJIAJIRI WENYEWE BADALA YA KUSUBIRI AJIRA SERIKALINI.
WAZIRI HUYO AMETOA USHAURI HUO KATIKA CHUO
KIKUU CHA ABRAHAMAN AL-SUMAAIT MEMORIAL CHUKWANI WAKATI WA
KUWATUNUKU SHAHADA YA UWALIMU WANAFUNZI WALIOHITIMU MAFUNZO HAYO
KATIKA MAHAFALI YA 14 YA CHUO HICHO.
AMESEMA
KUWA KUMEKUWA NA UPUNGUFU MKUMBWA WA AJIRA SERIKALINI, HUKU WAHITIMU
WAKIENDELEA KUONGEZA KILA MWAKA.
WAZIRI SHAMHUNA AMEUPONGEZA UONGOZI WA CHUO
HICHO KWA KUKIPANUA NA KUKIPA HADHI ZAIDI KUTOKA CHUO CHA ELIMU NA SASA KUWA
CHUO KIKUU KAMILI NA KUPEWA JINA JIPYA LA SUMAIT UNIVERSITY.
KATIKA KUKIIMARISHA CHUO KIKUU CHA SUMAIT
WAZIRI SHAMHUNA AMESHAURI KUONGEZWA FANI ZA UTAFITI NA MASUALA YA USHAURI
ILI KUKIPA HADHI ZAIDI NA KUTOA WANAFUNZI WALIOBORA.
AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUTUNUKU SHAHADA
KWA WAHITIMU, MWENYEKITI WA BARAZA KUU LA CHUO DKT. ABDULRAHMAN
AL-MUHAILAN ALIMPONGEZA KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO HICHO PROFESSA HAMAD
RASHID HIKMANY NA WASAIDIZI WAKE KWA KAZI KUBWA WALIOFANYA KATIKA KUKIFANYIA
MAGEUZI CHUO HICHO..
ALIISHUKURU SERIKALI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUPITIA KAMISHENI YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU) KWA
USHAURI NA MAELEKEZO MAZURI WALIOWAPA NA HATIMAE KUPATA USAJILI
KATIKA KAMISHENI HIYO.
AMEONGEZA KUWA HIVI SASA WANAIMARISHA IDARA
YA UCHAPAJI YA CHUO HICHO NA KUIENDESHA KIBIASHARA ILI
KUWAVUTIA WATEJA KUTOKA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI.
JUMLA YA WAHITIMU 266 WALIKABIDHIWA SHAHDA
ZAO KATIKA MAHAFALI HIYO NA KUFIKISHA IDADI YA WAHITIMU 1704 TOKEA
KUANZISHWA MWAKA 1998.
No comments:
Post a Comment