PEMBA.
WASTAAFU WA TAASISI ZA UMMA ZA SERIKALI YA JAMUHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAMETAKIWA
KUSHIRIKIANA KWA KARIBU KATIKA KUTUMIA UJUZI NA TAALUMA ZAO ZA MUDA MREFU NDANI
YA JUMUIYA WANAZOZIANZISHA BAADA YA KUSTAAFU KWAO ILI KUENDELEA KUCHANGIA MAENDELEO YA TAIFA.
WITO HUO UMETOLEWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR
BALOZI SEIF ALI IDDI WAKATI AKIZINDUA RASMI BODI YA WADHAMINI YA JUMUIYA YA
WASTAAFU PEMBA KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA TASAF ULIOPO
KATIKA MAJENGO YA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA.
BALOZI SEIF AMESEMA KUWA
MASHIRIKIANO HAYO YATATOA NAFASI NZURI KWA WASTAAFU HAO KUONDOA SHAKA YA
KUENDELEZA MAISHA YAO KUTOKANA NA BAADHI YAO KUPATA WAKATI MGUMU KABLA NA
BAADA YA KUSTAAFU KWA VILE WANAKUWA BADO HAWAJAJIPANGA.
AMEFAHAMISHA KUWA WAPO BAADHI YA WAFANYAKAZI WA TAASISI
ZA UMMA NA ZABINAFSI AMBAO WANAOGOPA KUSTAAFU WAKATI UTARATIBU WA KUFANYA HIVYO
UPO WAZI NA SAHIHI KUTOKANA NA MUONGOZO WA UTUMISHI SERIKALINI.
AKITOA TAARIFA FUPI KATIBU WA JUMUIYA YA WASTAAFU PEMBA
BWANA MAJID MOH’D AMESEMA KUWA JUMUIYA HIYO ILIYOANZISHWA MWISHONI MWA
MWEZI WA MEI MWAKA 2012 IMELENGA KUWATAKA WASTAAFU KUFANYA KAZI BADALA YA KUBWETEKA NA KUANZA TABIA YA
KUOMBA OMBA AMBAYO HAIPENDEZI KATIKA JAMII.
BWANA MAJID ALISEMA WANA JUMUIYA YA WASTAAFU PEMBA
WAMEPATA FARAJA KUTOKANA NA UONGOZI IMARA WA BODI YA WADHAMINI WA JUMUIYA
HIYO AMBAO UMEONYESHA UONI MPANA WA KUFIKIRIA KUBUNI MIPANGO NA MIRADI YA
KUIENDELEZA JUMUIYA HIYO.
MAPEMA AFISA MDHAMINI WIZARA YA KATIBA NA UTAWALA BORA
PEMBA NDUGU OMAR KHAMIS JUMA
AMESEMA KUWA JUMUIYA YA
WAFANYAKAZI WASTAAFU PEMBA INAFANYA KAZI KWA UMAKINI MKUBWA NA WIZARA
HIYO TOKEA KUASISIWA KWAKE MWAKA ULIOPITA.
JUMUIYA YA WAFANYAKAZI WASTAAFU KISIWANI PEMBA
IMEANZISHWA TAREHE 23 MEI MWAKA 2012 NA KUSAJILIWA RASMI MWEZI DISEMBA
MWAKA 2012.
No comments:
Post a Comment