ZANZIBAR.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeELEZEA YAKUWEPO Afisa muandamizi wa
cheo cha Naibu Kamishna wa Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) HAPA ZANZIBAR kwa
lengo la kusimamia ukusanyaji wa Mapato yaNAYOTOKANA na ushuru wa Fedha
na ushuru wa bidhaa katika juhudi za kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
USHAURI HUO UMETOLEWA na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee
wakati akijIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO
KINACHOENDELEA HUKO CHUKWANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
Amesema KUWA Mamlaka ya Mapato Tanzania
ni Taasisi ya Muungano iliyoundwa kwa mujibu wa sheria Na.11 ya mwaka
1985 ambapo inapaswa kuwa na Ofisi yake Zanzibar
Amesema kuwa kazi ya TRA Zanzibar
nikukusanya Mapato ya Muungano yanayotokana na kodi ya Mapato, Ushuru wa
ForOdha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini kama ilivyoainishwa na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Ameongeza kuwa kodi iNAYOTOkana na ushuru
wa Forodha inasimamiwa na Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya MWAKA 2004 na kwa mujibu wa sheria hiyo Zanzibar ni sehemu ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni moja kati ya sehemu ya nchi wanachAma
wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Waziri HUYO AMEFAFANUWA kuwa sheria
ya ushuru ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki imeweka utaratibu wa
uwekaji thamani Bidhaa zinazotoka Nje na Ndani ya Nchi Wanachama wa Jumuiya
hiyo.
No comments:
Post a Comment