tangazo

tangazo

Thursday, January 8, 2015

SHIRIKA LA HUDUMA ZA MAKTABA LATAKIWA KUPELEKA HUDUMA HIO VIJIJINI



PEMBA.

Shirika la huduma za Maktaba Zanzibar limetakiwa kuangalia uwezekano wa  kuzidisha kasi ya majukumu yake katika kupeleka huduma za maktaba Vijijini ili wananchi waweze kuongeza maarifa yanayokwenda sambamba na mahitaji ya maisha yao.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Maktaba Kuu ya Zanzibar Tawi la Pemba  KATIKA MAENEO YA Chachaani Chake chake KISIWANI Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya kusherehekea kutimia miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu wa Zanzibar ya Mwaka 1964.
Balozi Seif aMEsema KUWA anaFAHAMU juhudi zinazochukuliwa na shirika la huduma za Maktaba Zanzibar lakini kasi hiyo ni vyema kwa hivi sasa ikaelekezwa zaidi vijijini kUTOKANA NA  wananchi wengi wanaoishi katika maeneo hayo hawana fursa za kutosha za kujisomea na kujiendeleza.
AMEsema KUWA  hivi sasa huduma nyingi za maktaba zinapatikana zaidi katika maeneo ya miji ambako watu wengi wana maarifa pamoja na vyanzo mbadala vya kupata huduma hiyo kwa kujisomea na kuongeza maarifa yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali imefanya juhudi za kuongeza maktaba ikifahamu kwamba eneo hilo ni muhimu kwa  kuwapatia wananchi maarifa ya fani mbali mbali.
Balozi Seif alitoa wito kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu, magazeti na majarida kwa lengo la kuongeza maarifa mapya yatakayowasaidia katika maisha yao lakini pia ni sehemu ya kujiburudisha.
Mapema akisoma risala yenye mnasaba na shughuli hiyo ya Maktaba Kuu ya Zanzibar Tawi la Pemba Msaidizi Mkutubi Mkuu wa Maktaba hiyo Bibi Mwache Moh’d aMEsema  KUWA ujenzi wa jengo la Maktaba hiyo ulioanza mwezi Septemba mwaka 2013 tayari umeshafikia asilimia 90%.
Bibi Mwache aMEsema KUWA  ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika na kutoa huduma za Maktaba kwa wanafunzi, wataalamu na wananchi  mwezi ujao umezingatia mahitaji ya watu maalum WAKIWEMO WATU wenye ulemavu, watoto wadogo pamoja na watu wazima.
ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kugharamia ujenzi huo utaofikia jumla ya shilingi Milioni 655,000,000/- ambapo huduma za kijamii zitakuwa zimesogezwa kwa Wananchi.
KWA  UPANDE WAKE Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zahra ALI Hamad aMEsema KUWA Wizara hiyo hivi sasa imejikita kuelekeza nguvu zake katika ujenzi wa Maktaba za Wilaya ili kuwajengea utamaduni wa kupenda kusoma Wanafunzi na  Wananchi wa maeneo yote Mjini na Vijijini.

No comments:

Post a Comment