WILAYA YA KUSINI .
NAIBU WAZIRI WA MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO ISSA HAJJI
USSI GAVU AMESEMA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ITAENDELEA KUCHUKUWA
HATUA MBALIMBALI ILI KUWAPATIA WANANCHI MAENDELEO.
AKIZUNGUMZA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI CHUMVI KUWA
BARIDI HUKO KATIKA KIJIJI CHA UZI NG”AMBWA AMESEMA KUWA LENGO LA
SERIKALI NI KUWASOGEZEA WANANCHI WAKE WA MJINI NA VIJIJINI MAENDELEO YA
HARAKA ZAIDI ILI KUWAEPUSHIA USUMBUFU KATIKA KUFUATA HUDUMA ZA KIJAMII.
AMEFAHAMISHA KUWA MADHUMUNI YA MAPINDUZI YA MWAKA 1964 NI
KUJENGA MAISHA BORA ILI JAMII IWEZE KUONDOKANA NA DHULMA NA
UNYONGE WA WAKOLONI.
KWA UPANDE WAKE NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI MAKAAZI
MAJI NA NISHATI MUSTAFA ABUOD JUMBE AMESEMA UTEKELEZAJI WA MIRADI NI
KATIKA MATUNDA MAPINDUZI AMBAYO YAMETILIA MKAZO SUALA LA USAMBAZAJI
WA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA KWA WANANCHI WA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA.
HATA HIVYO AMEWAOMBA WANANCHI WA KIJIJI CHA UZI KUILINDA
NA KUITUNZA MIUNDOMBINU HIYO KWA KUSAMINI JITIHADA ZA SERIKALI ZA KUWASOGEZEA
MAENDELEO KATIKA SHEHIA HIYO.
MRADI HUO UMEGHARIMU JUMALA YA SHILINGI
MILIONI MIA NNE NA ARUBAINI NA TATU NA UNATARAJIWA KUWANUFAISHA ZAIDI YA
WANANCHI ELFU MOJA MIA MBILI WA KIJIJI CHA UZI.
No comments:
Post a Comment