wilaya ya mjini.
mkuu wa kitengo cha mambo ya dini wa kamisheni ya wakfu na mali ya amana
zanzibar fadhilatu sheikh ismail asaa kheri amewataka wazazi na walezi nchini
kuwashirikisha watoto wao katika mashindano yakuhifadhi qur-an .
sheikh ismail ametoa wito huo leo katika kongamano la jumuiya
yakuhifadhisha qur-an na kusimamia suala
la hijja yakinamama lililofanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari ya haile
salasie mjini zanzibar.
amewasisitiza waislam kuwasimamia watoto wao ili kuepusha kujishirikisha katika mambo maovu yaliyoletwa na utandawazi.
akizungumzia suala la utekelezaji
wa ibada ya hijja sheikh ismail amezitaka familia kuanzisha mfuko maalum wa
zakka ili kuweza kusafirisha mtu mmoja kila mwaka kwenda nchini saudiarabia
kutekeleza ibada ya hijja pamoja nakufanyiwa mambo mengine ya kheri.
hata hivyo alim huyo ameisisitiza jumuiya hiyo kuendelea na juhudi zake
zakuhifadhisha vijana wakiislam kitabu kitukufu cha qur-an sambamba nakuhimiza
utekelezaji wa mafundisho ya qur-an na sunna za mtume muhammad s.a.w kwa
vitendo.
No comments:
Post a Comment