ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Dkt. Ali
Muhamed Shein aMEwashauri wazazi na walezi kufanya jitihada ya
kuwaelimisha watoto historia za Maeneo wanayowatembeza.
Dkt. Shein aMEeleza hayo katika ufunguzi wa Kiwanja cha
kufurahishia watoto cha Uhuru kilichopo Kariakoo (ZSSF
Zanzibar TAG) ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
AMEsema kUWA KUTOKANA NA watoto
KUWA hazina Ya taifa la baadae wanahitaji kuelimishwa
mambo mbali mbali yanayohusu historia na kuandaliwa sehemu maalumu
za kupumzika ili KUPATA faraja baada ya saa za masomo.
AIDHA DR SHEIN AMEUPONGEZA Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kusimamia vyema ujenzi wa mradi
huo mkubwa wa kiwanja na kumalizika katika muda
uliopangwa.
Alitoa changamoto kwa ZSSF kupanua na kuuimarisha mfuko huo kibiashara
kwa kuanzisha miradi mikubwa ya uwekezaji na kuwahamasisha wafanyakazi wa
sekta binafsi kujiunga na kuwa wanachama wao.
KWA UPANDE WAKE Waziri wa Fedha ZANZIBAR NDUGU Omar Yussuf Mzee aMEeleza kuwa
ZSSF itaangalia bei za mapembeya ya kiwanja hicho ili watoto
wote waweze kuingia kufurahia matunda ya Mapinduzi yao.
NAYE Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Abdulwakil Haji Hafidh aMEsema KUWA
jumla ya shilingi bilioni 15 zilitumika katika ujenzi wa
kiwanja hicho cha Uhuru Kariakoo.
AMEsema KUWA walikabidhiwa rasmi kiwanja hicho na Wizara ya
Habari, Utamaduni Utalii na Michezo mwezi Agost 2008 na kuanza
ujenzi October 2012.
Kiwanja hicho kina mapembea kumi, Maduka ya Biashara 32, Ukumbi wa
kufanyia sherehe, eneo la kuegeshea magari na kunampango wa kujegwa
kituo cha Polisi hivi karibuni kwa lengo la kuimarisha ulinzi.
No comments:
Post a Comment