dar-es-salaam.
SERIKALI ya jamhuri ya muungano wa
tanzania imesema kuwa mradi wa ujenzi
wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila
nje kidogo ya mji wa Dar es salaam utagharimu Dola za kimarekani Milioni 61.
Katika mradi huo Tanzania imechangia
dola za kimarekani milioni 18 serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa mkopo wa dola za
kimarekani milioni 43 ili kufanikisha ujenzi wa chuo hicho katika eneo la
Mlonganzila mjini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya
kukamilisha ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho mjini Dar
es salaam Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa
amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani.
Dkt. Kawambwa amesema kuwa
mbali na ujenzi wa chuo hicho, serikali itajenga hospitali nyingine ya
Muhimbili ambayo ujenzi wake utamalizika sambamba na ujenzi wa chuo hicho ili
kuwawezeha wananchi kupata huduma bora za afya.
Amebainisha kuwa hospitali
hiyo itakapokamilika itakuwa kubwa
zaidi na yenye vifaa vya kisasa nakusaidia kupunguza msongamano wa
wagonjwa uliopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kuwasaidia
wanafunzi kupata sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo
cha Tiba Muhimbili Prof. Ephata Kaaya amesema kuwa mradi huo
umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikihusisha ujenzi wa
chuo cha tiba na Hospitali ya kisasa ya muhimbili na awamu ya pili
itakuwa ujenzi wa hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya Moyo na mishipa
ya fahamu.
No comments:
Post a Comment