WILAYA YA KATI.
WANANCHI WA
KIJIJI CHA MPAPA WILAYA YA KATI UNGUJA WAMEIOMBA SERIKALI
KUWATAFUTIA WAFADHILI WA KUMALIZA UJENZI WA KITUO CHAO AFYA ULIOKWAMA KWA ZAIDI
YA MIAKA KUMI NA SABA.
AKIZUNGUMZA NA
ADHANA FM RADIO KWA NIABA YA WENZAKE MMOJA WA WANANCHI HAO BI MARIYA
KHAMIS AMESEMA KUWA LICHA YA
KUPOKEA MISAADA MBALI MBALI YA UJENZI WA
KITUO HICHO BADO WANAHITAJI WAFADHILI ZAIDI ILI KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO
CHAO.
AMESEMA KUWA
KUKOSEKANA KWA KITUO CHA AFYA KIJIJINI HAPO KUNAWAPELEKEA KUPATA USUMBUFU
HUSUSAN KWA KINA MAMA WAJAWAZITO NA
WATOTO KUTOKANA NAKULAZIMIKA KUFUATA
HUDUMA HIYO KATIKA VIJIJI VYA MBALI VIKIWEMO MWERA, BAMBI NA UZINI.
HATA HIVYO
WANANCHI HAO WAMEIOMBA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU
MBALIMBALI KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO HICHO ILI KUEPUSHA MSONGAMANO WA
WAGONJWA KATIKA HOSPITALI ZA MIKOA.
No comments:
Post a Comment