DAR-ES-SALAAM.
JESHI LA POLISI NCHINI LIMESEMA KUWA Kufuatia kukamilika kwa mchakato wa
uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na kuendelea kwa
zoezi la kuapishwa kwa viongozi hao katika maeneo mbalimbali hapa nchini,
kumejitokeza tabia ya baadhi ya wananchi kufanya vurugu na fujo katika zoezi
hilo.
TAARIFA YA JESHI HILO ILIYOTOLEWA KWA VYOMBO VYA KHABARI NAKUSAINIWA NA MSEMAJI WA JESHI LA POLISI NCHINI ADVERA BULIMBA IMESEMA KUWA Baadhi ya wananchi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kufanya fujo na vitendo vya vurugu ikiwemo kuwapiga baadhi ya watendaji wanaosimamia zoezi la kuapisha na kuwapiga viongozi wateule waliochaguliwa kihalali na wananchi kwa madai kuwa hawakushinda kihalali katika uchaguzi huo jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini, liMEtoa onyo kwa wananchi wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake IWAPO mtu hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, KUfuatA utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake kATIKA ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Jeshi HILO liMEwataKA Wakurugenzi na Maafisa watendaji wenye dhamana ya kusimamia mchakato wa kuwaapisha wenyeviti waliochaguliwa, kufuatilia kwa karibu migogoro inayojitokeza na kuitatua mapema ili kuepusha migongano inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
BULIMBA AMESEMA KUWA JESHI LA POLISI halitamvumilia mtu aU kikundi chochote kitakachofanya vurugu KWA MADAI YA ushabiki wa siasa na badala yake atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

No comments:
Post a Comment