ZANZIBAR
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESHAURIWA KUWEKA MIKAKATI
MADHUBUTI KATIKA KUTOKOMEZA RUSHWA HAPA NCHINI,KWA LENGO LA KUEPUSHA MATATIZO
YANAYOSABABISHWA NA DHAMBI HIYO.
USHAURI HUO UMETOLEWA NA BAADHI YA WANANCHI
WAKATI WAKICHANGIA MADA KATIKA KIPINDI CHA NI WAJIBU WANGU KUSEMA,
KINACHORUSWHA HEWANI NA REDIO ADHANA FM.
WANANCHI HAO WAMESEMA KUWA BADO JUHUDI INAYOCHUKULIWA NA SERIKALI YA
ZANZIBAR KATIKA KUTOKOMEZA RUSHWA NI NDOGO.
MBALI NA HAYO WAMEWASIHI ASKARI WA BARABARANI KUACHA KUDAI RUSHWA KUTOKA
KWA MADEREVA,PALE WANAPOWAKAMATA MADEREVA HAO
KWA MAKOSA MBALIMBALI,ILI KULINDA USALAMA WA RAIA.
KWA UPANDE WAKE MMOJA WA WACHANGIAJI
HAO NDUGU SAID MUHAMED HAJI AMEFAHAMISHA KUWA,LICHA YA KUANZISHWA KWA TAASISI
KADHA ZA KUZUWIA RUSHWA HAPA NCHINI,TATIZO LA RUSHWA LINAONEKANA KUKUA SIKU
HADI SIKU.
No comments:
Post a Comment